
Kamanda mpya wa Vijana CCM Tawi la Bwawani kata ya Mwananyamala Steven Mengele Nyerere, akiongea na wana CCM. mara baada ya kutawazwa rasmi kuwa kamanda wa vijana wa kata hiyo leo kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za tawi hilo na kuhudhuriwa na wanachama wa chama hicho, pamoja na marafiki wa msanii huo anayeigiza sauti za viongozi. "Steve Nyerere" amewashukuru marafiki zake, wazee wake mtaani, mama zake pamoja na mama yake aliyemtaja kwa jina moja la Ritah. ambaye amemtania kwamba anaongea sana hivyo anaweza kuanzisha chama cha kuwasuta watu na kikawa kizuri sana, lakini pia hakusita kumshukuru mke wake na kumtania kwamba leo walipoamka asubuhi alimsalimia kwa kumtania na kusema "Mambo Kamanda naye Steve Nyerere akajibu Poa mke wangu"

Kamanda wa vijana wa CCM tawi la Bwawani Bw, Steven Mengele Nyerere akiwatambulisha wasanii wenzake katika mkutano wa kumsikika kama kamanda wa vijana wa tawi hilo kulia ni Steven Jacob JB, Dude na kushoto ni waigizaji Rich Richie na msanii Chikoka ambaye anagombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Ilala.

Mjumbea wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka Mkoani Mara na mgeni rasmi Bw. Domi Athman Juma akimvisha joho Kamanda mpya wa vijana wa tawi la Bwawani kata ya Mwananyamala Steven Mengele maarufu kama Steven Nyerere leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika tawini hapo na kuhudhuriwa na wanaccm mbalimbali wa kutoka tawi hilo.

Abbs Mwinyi akiongea katika mkutano huo mara baada ya kuchangia fedha ambazo hakutaka kutangaza kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya kamanda wa vijana wa Tawi hilo amabaye amesimikwa leo.

Toto wa rais Msytaafu Ali Hassan Mwinyi akingia katika eneo la mkutano huo huku akiwa ameongoza na Risasi Mwaulanga anayejulikana kama balozi wa Amani Afrika.

Wanaccm wakiwa wamekaa wakimsikiliza mgeni rasmi Bw. Domi Athman Juma ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu Taifa wa CCM wakati alipokuwa akiongea jukwaani.

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Tawi la Bwawani Kata ya Mwananyamala wakichezu muziki wa Taarab wakati wa kumsimika kamandawa vijana wa tawi hilo Bw. Steven Mengele (Nyerere) kwenye mkutano uliofanyika tawini hapo.
No comments:
Post a Comment