
Mnara wa bia ya Ndovu Special Mart wenye kuonyesha sehemu ya alama ya mafanikio unavyoonekama mara baada ya kuzinduliwa leo.

Mnara wa Ndovu Special Mart ukizinduliwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia Tanzania (TBL),
Robin Goetzsche akifafanua jambo kuhusu bia ya Ndovu Special Mart huku akiwa ameshika chupa ya kinyaji hicho katika uzinduzi wa mnara wa bia hiyo leo wenye kuonyesha sehemu ya alama ya mafanikio uliopo maeneo ya Namanga jijini Dar.

Meneja wa Bia ya Ndovu Special Mart,Oscer Shelukindo akielezea namna walivyoweza fanikiwa kupata tuzo ya ubora wa bia kutoka kitivo cha upimaji na ubora (Monde Selection) ambao bia ya Ndovu Special Mart iliupata huko nchini ujerumani ambapo kwa kulienzi hilo kampuni ya bia ya TBL iliweza kutengeneza mnara mkubwa katika maeneo ya Namanga jijini Dar unaoonyesha mfano wa chupa ya bia hiyo uliozindiliwa rasmi leo.

Mpishi mkuu wa kampuni ya bia Tanzania (TBL),Mzee Gaudence Mkolwe nae aliongea machache kuhusu bia hiyo katika uzinduzi wa mnara wenye kuonyesha sehemu ya alama ya mafanikio wa bia ya Ndovu Special Mart,uliozinduliwa leo jijini Dar.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bia Tanzania (TBL),
Robin Goetzsche (kati) akigonganisha chupa na Meneja wa Bia ya Ndovu Special Mart,Oscer Shelukindo (kushoto) pamoja na Mpishi Mkuu wa kampuni hiyo,Mzee Gaudence Mkolwe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mnara wa bia hiyo ya Ndovu Special Mart uliopo Namanga jijini Dar.
Burudani ikiendelea kabla na baada ya uzinduzi huo.

Kaka Efraim Kibonde (kati) akiwa na Dj Choka (kulia) pamoja na Mdau.

Wadau wa TBL wakigonganisha chupa ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Mnara huo.

Wadau wa habari wakibadilishana mawazo katika uzinduzi wa mnara huo leo.

Viongozi wa Juu wa TBL wakifuatilia uzinduzi huo.

wadau mbali mbali waliofika katika sehemu iliyoandalia kwa ajili ya uzinduzi wa mnara wenye kuonyesha sehemu ya mafanikio wa bia ya Ndovu Special Mart,wakishuhudia uzinduzi huo leo katika maeneo ya Namanga jijini Dar.
hiyo ni ndovu malt sio mart. mdau wa texas
ReplyDelete