
msela akijichukulia zake mabaki ya mafuta katika gari kama vile ni ya kwake na huu umekuwa ni utaratibu wa jamaa hawa pingi gari hizi ziwapo katika foleni au zikiwa zimesimama.

jamaa akiendelea na shughuli yake huku tandiboi wa gari hilo akiingia zake gari na kufanya kama hajamuona vile huyu msela.

hivi kwa swala hili ni nani anapaswa kuwawajibisha hawa jamaa wanaofanya shughuli hizi katika mabarabara na kama si kulitokomeza kabisa??maana wakati mwingine wanasababishaga madhara makubwa sana.
Hapo itakuwa washalipana hapo ukiwapelekea wenyewe picha japo sio vizuri kumfanya mtu afukuzwe kazi ila lazima aambiwe inaweza kuleta hatari si kwa huyo jamaa hata magari ya pembeni kukitokea mripuko..
ReplyDeleteKajima kunakipindi wafanyakazi walikuwa wanabeba kokoto wanaenda kuwauzia watu kwenye nyumba za ujenzi siku ya malipo wakaambiwa mshajilipa kumbe wale wa Japan walikuwa wanawachukuwa kwa Video nyumba wanazoenda kuuza. othman Michuzi kazi unayofanya ni nzuri kuliko wanaotakiwak ufanya upelelezi.