Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Butallah akiongea na waandishi wa habari pamoja na wanafunzi washiriki wa mchezo wa Pool katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa kampuni ya bia TBL,Ilala mchikichini jijini Dar.wengine ni Mwenyekiti wa mchezo wa Pool Taifa (TAPA),Isack Togocho (kushoto) na Katibu Mkuu wa mchezo wa Pool Taifa,Amos Kafwinga.
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Fimbo Butallah akikabidhi fedha ya usafiri kwa Naibu Waziri wa Michezo wa timu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Kayumba Torokoko.kushoto ni Wariri wa Michezo wa Chuo Royal (RCT),Robert Latonga.

**********************************
**********************************
HIGHER LEARNING SARARI LAGER POOL COMPETITION 2010
Bia ya Safari Lager, inayozalishwa na Tanzania Breweries Limited (TBL) na ambayo ndio mdhamini mkuu wa mchezo wa pool hapa nchini imetangaza kuanza kutimua vumbi kwa mashindano ya mchezo wa Pool kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu vya jiji la Dar es Salaam.(Higher Learning Safari Lager pool Competitions).
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya ijumaa may 14 hadi may 16,2010 kwenye fukwe ya Coco Beach ambapo vyuo shiriki vitatoana jasho kwenye mitanange ya kumsaka bingwa kihistoria wa mashindano hayo jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Michezo na Burudani,Mh. Joel Bendera ndie atakuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Meneja wa bia ya Safari Lager, Fimbo Butallah alisema “Azma ya Safari Lager ni kuleta mapinduzi ya kweli na mafanikio makubwa katika mchezo wa pool hapa nchini ambapo sasa mchezo huo umeingia katika hatua ya juu zaidi, udhamini huu wa mashindano vyuo vya elimu ya juu ni sehemu ya mikakati ya bia ya Safari Lager ya kufanya mcehzo huu kuwa na hadhi ya juu na hatimae kuweza kupata timu bora ya kuweza kuliletea Taifa letu heshima kubwa kwenye nyanja ya michezo ya ndani na kimataifa.
Akieleza juu ya maandalizi ya mashindano hayo,Bwana Butallah alisema vyuo vimejiandaa vyema ikiwa ni pamoja na kupatiwa semina juu ya kanuni na sheria zitakazotumika kwenye mashindano hayo ambapo leo Safari Lager imekabidhi tshirt na fedha za usafiri kwa kila timu itakayoshiriki.
Kwa upande wao viongozi wa vyuo shiriki,walitoa shukrani kwa Safari Lager kwa kusema “Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa bia ya Safari Lager na TBL kwa ujumja kwa mchango wao katika kuhakikisha mchezo huu wa Pool unakuwa na kupata hadhi ya juu hapa nchini hasa uamuzi wao wa kuamua kuyaratibu na kuyaandaa mashindano haya kwa vyuo vya elimu ya juu jijini Dar es Salaam na hivi leo mchezo wa Pool umekuwa na taswira tofauti na yenye matumaini makubwa hapa nchini Tanzania.”
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ni watengenezaji na wauzaji wa bia, vinywaji vya matunda vyenye asili ya kilevi (AFB’s) na visivyo na kilevi ndani ya Tanzania. TBL inazo hisa pia katika Tanzania Distilleries Limited na kampuni shirika, Mountainside Farms Limited.
Bia maarufu za TBL ni pamoja na Safari, Kilimanjaro, Ndovu Special Malt na Castle.Vinywaji vingine vya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redds Premium Cold.
TBL imo pia katika Soko la Hisa la Dar es Salaam na imeajiri watu kiasi cha 1,300 huku ikiwa na wawakilishi katika sehemu kubwa na Tanzania na viwanda vitatu vya bia na depot nane kwa ajili ya kusambazia bia na vinywaji vingine vya kampuni hiyo.

No comments:
Post a Comment