HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 13, 2010

Club Bilicanas Al Manusura Leo

wapenzi wa muziki wa bendi ya Twanga Pepeta wakiwa nje ya jengo la Club Bilicanas mara baada ya kutokea kwa shoti ya umeme iliyotokana na moja ya TV zilizomo ndani humo ambayo iliungua na baadae kufanya kitu kama mlipuko na kupelekea mtafaruku mkubwa sana kwa kila aliekuwemo ndani ya Club hiyo kutoka nduki bila kujua kwamba aliweza wezaje kufika nje.hali hii imetokea usiku huu wakati Bendi ya wana wa Kutwanga na Kupepeta ikiendeleza libeneke lake la kila Jumatano kupiga katika Club hiyo.
Askari waliweza kufika mapeka katika tukio hilo na kuhakikisja swala zima la usalama linapatikana kwa kila aliekuwepo eneo hilo
gari ya faya nayo ilifika eneo la tukio.
baada ya kuambiwa kuwa kila kitu kiko sana na muziki unaendelea kama kawa,basi kila mtu alitaka kuingia tena ndani kuhakikisha mkwanja wake unamalizika kihalali.

1 comment:

  1. Vitu vingine tunavikosea timing, wakati tatizo hilo linatokea BILICANAS ningekua hapo ningeweza kutoka na visimu viwili au vitatu .... nimepitwa.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad