HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 6, 2010

Mzee Wa Libeneke Alivyomwaga Chehe Kwenye Mkutano Wa Diaspora 2



Katika kongamano la Watanzania wanaoishi nje ya nchi lililofanyika nchini Uingereza mwishoni mwa mwezi wa Machi 2010, mwanablogu mahiri na mmoja wa waasisi wa ulimwengu wa kublogu kwa Watanzania, bwana Muhidin Issa Michuzi, alipata heshima ya mwaliko wa kuhudhuria na vile vile fursa ya kuzungumza katika kongamano hilo. Pamoja na mengi aliyoyazungumza, bwana Michuzi, al maaruf Ankal au Mdau wa libeneke, aligusia juu ya umuhimu wa kuthamini michango ya blogu mbalimbali katika ulimwengu wa mawasiliano. Vile vile aligusia juu ya umuhimu wa kuunganisha nguvu kwa wanablogu na zaidi sana, kuhamasisha Serikali na vyombo mbalimbali kutambua rasmi sekta hii muhimu ya mawasiliano.

Mdau
Subi
www.wavuti.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad