Kwako mzee wa libeneke la mtaa kwa mtaa,
habari za majukumu ya kila siku na tunakushukuru sana kwa kutuhabarisha mengi ya huku uswazi kwetu.mkuu naomba unianikie hiki kimkasa ili mchango wa wadau uweze kuchukua nafasi yake.
Kuna rafiki yetu mmoja ambaye anaumwa sana tangu mwishoni mwa mwaka wa jana na amehangaika kutafuta matibabu karibia hospitali zetu kuu zote za bongo bila mafanikio wakisema kwamba hawaoni ugonjwa.
Lakini kwa bahati nzuri mnamo mwezi wa 12 mwaka jana alipatikana daktari mmoja ambae aliweza kumcheki na kugundua tatizo lake yule mgonjwa na kukubali kumfayia matibabu mgonjwa huyo( Daktari huyo anafanyia shughuli zake pale Hospital ya Tumaini na Muhimbili),alisema angemfanyia kwa gharama ya sh. 250,000/- (laki mbili na nusu) kwa ajili ya kumafanyia operesheni mgonjwa huyo.
Ndugu na jamaa waliposikia hivyo ikabidi kila mmoja wetu kuzama mfukoni na kupiga donee ili huyo rafiki yetu aweze fanyiwa matibabu ya haraka.katika ile donee ilipatikana sh. 160,000/- (laki na sitini elfu) na akakabidhiwa kaka wa mgonjwa ili aendeleze hilo libeneke la donee mpaka itimie hicho kiasi alichokihitaji yule Daktari.Sasa kutokana na hali ya mgonjwa kuzidi kuwa mbaya hadi kufikia kumfanya Daktari yule kumuonea huruma mgonjwa yule ikabidi awaambie ndugu wa mgonjwa yule kwamba walete kile walichonacho kwa wakati huo ili aweze kumfanyia matibabu yule mgonjwa ili aweze kumuokolea maisha yake.
Sasa alipofatwa yule kaka wa mgonjwa ili kuweza kutoa ile hela ili mdogo wake akatibiwe matibabu.jamaa anasema hana hata senti tano (inamaana kazitungua zoote) na mgonjwa ndio anazidi kusota tuu home kwao kwa kukosa matibabu tangu mwezi wa 12 mpaka leo hii.
Hivyo sisi kama marafiki wa karibu wa yule mgonjwa tumeanza kuchanga tena jana ili mwenzetu akapate matibabu.sasa wadau naombeni mnisaidie kuhusu nini kifanyike kwa huyu kaka wa rafiki yetu ambaye amezitungua hela zote za kuweza kufanyia matibabu ya nduguye na ili hali akiona kabisa hali ya nduguye ilivyokuwa mbaya.
TUMFANYEJE HUYU JAMAA WADAU???
MAANA HANA UBINADAMU HATA KIDOGO
Mdau Mkereketwa
wa
Mtaa Kwa Mtaa Blog
aiseee poleni sana ndugu jamaa na marafiki, sasa nauliza huyo kaka yake kama bahati mbaya akamkosa ndugu yake hivi atalia kweli msibani? maana hapo itakuwa kama yeye ndio kamnyonga
ReplyDelete