HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 2, 2010

Chadibwa Beach Kutawaka Moto Pasaka Hii


Kwa mara nyingine wakazi wa Kigamboni watapata burudani katika siku tatu za Pasaka ambayo inaratibiwa na Club ya Chadibwa.Burudani hiyo ambayo inajumuisha disco la kila jumamosi, ambapo kutokana na sikukuu yenyewe uongozi umeamua kuongeza siku ya Jumapili na Jumatatu.

Akizungumza mmoja wa viongozi wa Klabu hiyo Robert Mwafrika amesema kuwa wameamua kuwaletea burudani wakazi wa Kigamboni ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakivuta kufuata burudani upande wapili.

"Tumeamua kuwaletea burudani ambayo kwa sasa ni Disco pekee linapigwa Beach kabisa huku kukiwa na ulinzi wa kutosha na Disco lenyewe linaletwa na Ma Dj wenye uzoefu, DJ John Dilinga aka Everlasting Dj JD, akishirikiana na DJ machahari kwenye machine DJ Q pamoja na DJ Juicy ambao kwa pamoja huwa wanafanya usiku kuonekana mfupi" alisema Mwafrika.

Aidha akifafanua Robert amesema kuwa siku ya Jumapili kutakuwa na Disco Toto kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 12 jioni kabla ya kuanza Disco la watu wazima kuanzia saa tatu usiku.

Kama hiyo haitoshi mambo ya vilaji na vinywaji uongozi umehakikisha watu wataburudika vyakutosha.Chadibwa ikishirikiana na Fire Burn Disco Theque walianza kupiga muziki wiki iliyopita ambapo inasemwa ilikuwa na mafanikio na muitikio mzuri sana na Disco hili litakuwa ni la kudumu kila Jumamosi ambapo mashabiki watapata burudani

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad