HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 24, 2010

Uozo Hospitali Ya Mwananyamala.

Habari Mzee wa Mtaa Kwa Mtaa,natumai uko poa na unaendeleza vyema libeneke la Mtaa Kwa Mtaa.

Naomba uiweke hii Taarifa yenye masikitiko makubwa sana katika Blog yetu hii ili kila mdau aweze kuipata taarifa hii,maana hali ni Mbaya sana katika Hospital ya Mwananyamala sijui hata ni mdudu gani mbaya alieikumba Hospital hiyo.kwa hakika hii nchi ndio maana inazidi kulaanika siku hadi siku.

Kwa walioangalia kwenye ITV taarifa ya habari imesikitisha saana kuona wagonjwa wakiwa kwenye ambulance wakisubiria wengine wazidiwe ndipo wapelekwe muhimbili.

Mh meya wa kinondoni SALUM LONDA akiwa na wenzake waliamua kuwatoke gafla bila taarifa hospital ya mwananyamala na kukuta wagonjwa wamelala kwenye ambulance ati wakisubiri ijae wapelekwe MUHIMBILI... jamani kweli hawa watu wanamjua MUNGU kweli..

Je ingekuwa ndugu yako anaumwa kweli wewe DK MKUU,DK SULEIMAN ulietetea ati ni kutokana na kufanya ECONOMY ya Mafuta ya Gari...???kweli wewe baba Mama yako ameletwa hapo amezidiwa anatakiwa kwenda muhimbili nyie si ndio mnakuwa wa kwanza kulazimisha dereva amwahimishe muhimbili iweje wengine mnawafanya kama Samaki wa MUSOMA jamani...??

Gari aiondoki mpaka ijae ndio safari ya kupeleka samaki inaanza..sasa binadamu hawana aibu wala haya kabisa jamani...Huyu dk bila haya wala aibu ya kuzaliwa alijitetea kwamba Hawakuwa na mafuta ya kutosha katika gari so wana minimize kwenda mara kwa mara kwa kusubiri wengine wajae wanaoitajika kwenda hospital.... .

Hivi Mh.Waziri wa afya inakuwaje unawapa kazi watu kama hawa?? watu wanaonekana kuwa sio wazima kabisa katika akili zao??na kama kweli wanayosema ya mafuta machache kwenye magari wewe na Wizara yako mnayafahamu hayo??na kama mnayafahamu kwanini mnayaangalia tuu??mnawaambia wasubirishe watu wanaohitajika opereshen kwenye ambulance;;; shame tanzania gov...,.

Yaani kwakweli kabisa hii hawa watumishi wa Hospital ya Mwananyamala ilitakiwa watolewe woote na kuletwa wengine wapya kabisa maana haiwezekani kila siku ujinga,ukatili,uozo,uuaji na uzembe uwe unafanyika katika Hospital hiyo hiyo tu na bado watu wanaangalia tuu.

Mh. Waziri tunaomba ulifanyie kazi swala hili,maana kama itaendelea kuwa hivi basi kila siku tutaendelea kuwapoteza ndugu zetu kwa uzembe mkubwa ufanyikao katika Hospitali ya Mwananyamala.

Watanzania tunahitaji kubadilika kudai haki zetu hata kwa damu

Mdau
mwenye Machungu.

3 comments:

  1. kweli kabisa mdau mwenye uchungu , mie nadhani kweli sisi wananchi tunahitaji majibu sahii kutoka kwa wa wakuu wetu serikalini , kuna waziri mkuu, waziri wa afya ,katibu mkuu,mganga mkuu wa mkoa , mganga mkuu wa wilaya na mganga mkuu wa hospitali [watendaji wakuu] ..hao wote wanakula kodi yetu tuna haki ya kupata majibu kutoka kwao kweli i haki kumwacha mgonjwa aliyezidiwa asubiri mpaka gari lijae ndio apelekwe rufaa ? ..hivi kweli wadanganyika hatuoni kijana obama jinsi alivyokazania kubadilisha mfumo wa bima ya afya kwa wote mpaka ikapitishwa ?Kwa wale wanaopenda kuangalia movie waangalie sinema ya Denzil inayoitwa "John Q" and its true story kuona watu ambao wanaweza kujitolea maisha sababu ya wajinga wachache wanashindwa kutoa huduma kwa jamii kwa kisingizio fedha hazipo! its the same to Mwananyamala Hospital clauds juzi asubuhi ilikuwa Topic ambayo kwa kweli aina jibu ...ndugu zangu wandanyanyika tutafika kweli kwa style hii ???

    ReplyDelete
  2. hii kali ya karne, mwakyembe alipata ajali ya gari iringa ndani ya lisaa ndege maalum ilifika kumchukua na kumpeleka dar kwa matibabu zaidi. sijui mil 15 za kodi ya mwezi kwa nyumba ya spika zingenunua lita ngapi za mafuta

    ReplyDelete
  3. hiyo ni usafiri, je wadini kewnye kupewa huduma inakuwaje kama ndio zao za kubana matumizi kwa uhai wa watu? huyo mganga mkuu aachishwe kazi, yuko wapi mkuu wa wilaya huko bukoba aliyechapa waalim viboko kwa uzembe? bora apewe kazi hapo mwananyamala na hospt nyingine ambazo mtu hupewi huduma bila kutoa chochote wasio na mtoa chochote ndio hufa haraka.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad