HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 1, 2010

TAARIFA TOKA KWA MH.ZITTO KABWE

Zitto Kabwe, Mb.
Kigoma Kaskazini.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika Gazeti la Mwananchi na The Citizen ya leo Jumatatu, Tarehe 1/3/2010 kuna habari ya kwamba ninatafakari kugombea ubunge katika Jimbo la Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam. Nimeona ni vema nitoe taarifa rasmi juu ya jambo hili.

Nimeunda kamati ya uchunguzi (Exploratory Committee) ya watu watatu kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina juu ya jimbo gani nigombee Ubunge katika uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka 2010. Majimbo ambayo nimeomba wayaangalie ni pamoja na Kigoma Kaskazini (ukiondoa kata ya Mwandiga ambayo imependekezwa kukatwa na kupelekwa Jimbo la Kigoma Mjini na hivyo kuondoa zaidi ya wapiga kura 15, 000 kutoka jimbo la Kigoma Kaskazini la sasa), Kigoma Mjini, Kahama, Kinondoni na Geita.

Nimeelekeza kufanyike utafiti (survey) wa kina ili nitakapofikia kufanya maamuzi nifanye maamuzi kutokana na taarifa za kutosha. Tutatumia wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya utafiti huo katika majimbo hayo na pia kwa ajili wa uchambuzi wa hali ya kisiasa na kutoa mapendekezo.

Ninatarajia kutangaza rasmi Jimbo nitakalogombea Ubunge mnamo siku ya Jumapili tarehe 28/3/2010.
Naomba ifahamike kuwa bado sijafanya uamuzi rasmi na kwamba uamuzi wangu utazingatia taarifa ya uchunguzi, ushauri wa viongozi wa chama changu (CHADEMA) na matarajio yangu ya kisiasa ya baadae. Ni muhimu kusisitiza kuwa nikiwa Mtanzania nina haki ya kugombea Ubunge mahala popote nchini.

Uamuzi wowote nitakaoutoa utazingatia kwa kiasi kikubwa sana umuhimu wa kujenga mfumo imara wa demokrasia ya vyama vingi na hasa kuwa na Bunge imara lenye wabunge wengi wa kambi ya upinzani.

(imesainiwa)
ZZK.
1/3/2010

1 comment:

  1. Ukiskia mtu anaenda shule lakini haelimiki, hii ndio dalili yake. Pamaoja na kwamba kama Zito anavyosema sheria inamruhusu kugombea ubunge mahala popote Tanzania, kutokuw ana msimamo ugombee wapi na loyaliti yako iko wapi ni upungufu wa hali ya juu sana.

    Hii ni moja ya sababu watz wengi hawawachagui wapinzani kisha wapinzani wanazani ccm wezi wa kura au wananchi ni wajinga hawaoni ccm hawafai na kwanini wanawapigia kura ccm.

    I just do not get it!

    ReplyDelete

Post Bottom Ad