Mambo vipi mkuu Othman,
Hongera sana kwa kusherehekea sikukuu yako ya kuzaliwa japo kekizz ulikula ukiwa umejifungia chumbani,lakini poa tu mkuu.
Sasa kaka kuna kitu nataka kukiuliza hapa Mtaani ili wadau wanisaidie kujibu maana mie hii kitu nimetoka kapa kabisa.
Inshu yenyewe iko hivi,eti kwa mfano wewe umeenda nyumbani kwa mtu ambako wewe kule uko ugenini na kwa bahati nzuri unafika tu na wenyeji wako ndio wanaanda msosi mezani na unakaribishwa bila hiyana mtu mzima unachukua zako udhu (unanawa mikono),sasa kabla hujaanza kutia ndani ghafla unaananza kusikia kiu na unaamua kuomba maji bila kusema maji ya namna gani.
Fasta fasta anaamka mtu na anakuletea ya kunawa na anakushikisha na soap mkononi.sasa Je,utanawa kuashiria kama umeshiba au utakomaa kwenye msosi??
Hilo ndilo swali lenyewe kaka,limwage hapo Mtaani ili wadau walichangie.
Mdau Mtaa Kwa Mtaa
Kisiju.
si utawaambia kuwa mimi nimeagiza maji ya kunywa sio ya kunawa!!! hilo ndio jawabu usione noma mshikaji!! mdau uk HPDL.
ReplyDeleteutawaambia kuwa umeomba maji ya kunywa. pia sio vzr kula kila unapokaribishwa mara nyingine wanakujaribu tu. hivyo acha ulafi
ReplyDeleteKwanini ula ikiwa kilipohandariwa hukuwepo?
ReplyDelete