HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 5, 2010

Mahakama Nchini yamuenzi aliyekuwa Jaji Mkuu wa Kwanza Tanzania!!

Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akikata utepe kuzidua jengo la kumbukumbu ya Jaji Mkuu wa Kwanza Mzalendo, Hayati Augustine Said kwenye mahakama ya Rufani jijini Dar es salaam March 5, 2010. Wapili kushoto ni Jaji Mkuu Mh. Augustine Ramadhan na kushoto ni Jaji Kiongozi Mh. Fahiki Jundu
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizindua jengo la kumbukumbu ya Jaji Mkuu wa Kwanza Mzalendo, Hayati Augustine Said kwenye mahakama ya Rufani jijini Dar es salaam leo.Wapili kulia ni Jaji Mkuu,Mh. Augustine Ramadhan na kulia ni Jaji Kiongozi ,Mh. Fakihi Jundu.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Augustine Ramadhan (kushoto) kabla ya kuzidua jengo la kumbukumbu ya Jaji Mkuu wa Kwanza Mzalendo, Hayati Augustine Said kwenye mahakama ya Rufani jijini Dar es salaam.(katikati) ni Jaji Kiongozi Mh. Fakihi Jundu.
Jaji Mkuu wa Tanzania ,Augustino Ramadhan

Na Benjamin Sawe,Maelezo
Dar es Salaam

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amempongeza Jaji Mkuu wa Mahakama nchini Augustino Ramadhani kwa uamuzi wa Kujenga jengo jipya la Mahakama nchini kama ishara ya kumbukumbu ya aliyekuwa Jaji Mkuu wa kwanza Hayati Jaji Augustine Saidi.

Waziri Mkuu alisema kitendo alichofanya Jaji Ramadhani cha kutumia bajeti aliyotengewa na Serikali ya kutengeneza makazi yake na kuamua kujenga jengo la mahakama ya Rufani ni cha kuigwa na viongozi nchini.

“Uamuzi ulioufanya wa kutumia fedha ulizotengewa na Serikali kwa ajili ya kujenga makazi yako ya kuishi na kuamua kutumia bajeti hiyo kwa ujenzi wa jengo la mahakama ni cha mfano wa kuigwa kwani umeonyesha uzalendo”.

Alisema Waziri Mkuu Waziri Mkuu alisema katika zama hizi viongozi wengi huweka maslai yao kwanza na kuyaacha maslahi ya taifa hivyo kudumaza maendeleo ya nchi.Awali Jaji Mkuu Agustino Ramadhani alisema ameamua kujenga Jengo hilo na kutengeneza sanamu ya aliyekuwa Jaji Mkuu wa kwanza Tanzania Hayati Augustine Saidi ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake kwa mahakama.

Akizungumzia wasifu wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa kwanza Tanzania Hayati Augustine Saidi Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Jaji Luis Mkame alisema Hayati Augustine Saidi alikuwa muwajibikaji katika shughuli za mahakama.

Jaji Luis Makame alisema Hayati Saidi alikuwa mshauri mzuri katika mambo mbalimbali ya kimahakama na hata nje ya mahakama hivyo kuboresha hali ya kiutendaji wa mahakama nchini.

Akitoa shukrani kwa niaba ya Familia mtoto wa Hayati Jaji Augustine Saidi Bwana Daniel Augustine Saidi aliishukuru Serikali pamoja na mahakama kwa kitendo cha kujenga jengo la mahakama na kuweka sanamu ya baba yao kama ishara ya kumbukumbu ya mpendwa wao.

“Kwa niaba ya Familia tunapenda kutoa shukrani zetu kwa Jaji Mkuu Agustino Ramadhani kwa kujenga jengo jipya pamoja na kutengeneza sanamu ya baba yetu kama ishara ya kumbukumbu ya kumuenzi”.Alisema.

Jaji Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika, Augustine Saidi, alifariki dunia tarehe 19 mwaka 1995 nyumbani kwake Msasani mjini Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 66.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad