
Vipande hivyo vya mayai ya mbuni vinasemekana kuwa na michoro inayoashiria kwamba binadamu alianza kuwasiliana kwa lugha ya ishara (symbolism) miaka mingi sana iliyopita. Wanazuoni hao ambao wamekuwa wakichunguza suala hilo tangu mwaka 1999 katika taasis ya National Academy of Sciences wamesema kwamba kuna uwezekano mkubwa sana kuwa huu ni uthibitisho kwamba binadamu hawakuanza leo kutumiana ujumbe kwa njia ya alama.
Dr. Pierre-Jean Texier anasema jumbe hizo ziliwasilishwa katika mtindo wa mistari iliyokwaruzwa katika nyuso za mayai ya mbuni ili kupeleka taarifa kwa wahusika. Huu ni uthitisho tosha kwamba SMS au ujumbe mfupi wa maneno si jambo jipya bali ni mwendelezo wa utamaduni ulioanza maelefu ya miaka iliyopita tangu binadamu kuwasili duniani kwa mara ya kwanza.
Texier, akiongea na BBC, anasema jumbe hizi katika mayai ya mbuni huenda zilitumika kutambulisha kabila na desturi za watu fulani. Mawasiliana kwa njia ya alama kama michoro na herufi, ambazo humaanisha kitu tofauti na kile unachokiona kwa macho na hatimae kumpa binadamu ujumbe fulani, ndio kitu kinachofanya binadamu awe mnyama wa tofauti na wanyama wengine wote ulimwenguni.
Wanazuoni hawa kwa sasa wanaumiza vichwa vyao kufahamu ni mahala gani hasa matumizi ya alama kwa ajili ya mawasiliano ililtumika kwa mara ya kwanza kabisa. Walishawahi kuvumbua mikufu ya magamba ya konokono katika mapamngo ya Skhul huko Israel na Oued Djebbana huko Algeria. Mikufu hiyo inasadikiwa kuwa na umri usiopungua miaka kati ya 90,000 na 100,000.
Kweli tuna mengi ya kujifunza, dunia ni bonge la Maktaba.
No comments:
Post a Comment