HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 24, 2010

Vyombo Vya Habari Kushirikishwa Na Jeshi La Polisi Katika Kutokomeza Uhalifu


Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi hapa nchini, wameagizwa kutoa ushirikiano na kujenga ubia na Waandishi wa Habarí ili kuwawezesha kutekeleza wajibu wao kama wadau muhimu wa kiutendaji Kitaifa.

Agizo hilo limetolewa na Makamishna wa Polisi kwenye mkutano wa Maafisa Wakuu wa Jeshi hilo mjini Dodoma wakati wa mjadala juu ya ushirikishwa wa Vyombo vya Habari katika kuwaelimisha wananchi kuhusiana na mpango wa Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai nchini Kamishna Robert Manumba, amesema kuwa ni wajibu wa kila Kamanda wa Polisi hapa nchini, kuhakikisha kuwa anatoa ushirikiano unaostahili kwa waandishi hao ili nao wawezesha kutimiza wajibu wao wa kuwaelimisha wananchi juu ya yale yanayotokea kila siku.

Naye Mkurugenzi wa Operesheni wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Paul Chagonja, amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa waandishi bandia maaruka kama Makanjanja, ipo haja ya kila mmoja wao kuwa na Kitambulisho cha Chombo anachokifanyia kazi pamoja na kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Press Card) ili kuondoa utata.

Amesema utaratibu huo ukifuatwa kutapunguza furusa ya kuwepo kwa waandishi bandia ambao wamekuwa wakichafua uhusiano uliopo baina ya Jeshi la Polisi na Biombo vya Habari kwa waandishi wasio wajibika popote kuandika abarrí za uchochezi ama zinazowachafua vatu fulanifulani.

Kwa upande wake Mkuu wa Mipango na Bajeti kwenye Jeshi hilo Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP John Masawe, amesema ipo haja ya Waandishi wa Habari nao kupewa mafunzo juu ya mpango wa Polisi jamii ili waweze kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya mpango huo.

Kamanda Masawe amesema kuwa waandishi wakielimishwa itakuwa ni msaada mkubwa kwa Jeshi la Polisi katika kueneza mpango wa Polisi Jamii kwa wananchi katika kutoa taarifa za kihalifu.Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, amewataka Makamanda kutogombana na Waandishi wa Habari na badalayake wahakikishe wanashirikiana kwa kuwapa taarifa sahihi na kwa wakati muafaka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad