HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 2, 2010

Mjadala Wa Haja Toka Kwa Mdau,Kuhusiana Na Lililotokea Kwa Jerry Muro

Habari za kazi ndugu zanguni na poleni na majukumu na heka heka za kuchapo! Binafsi ninamuunga mkono kaka yangu Mgeta kuwa suala la urafiki na miliki za vifaa sidhani kama zinaweza kuwa na sababu ya kuzijadili hapa. Cha msingi kwa sasa ambacho tunapaswa kufuatialia ni hili sakata zima, na tunapaswa kulijadili kwa umakini kutokana na hali halisi ya nchi ilivyo hivi sasa.

Nasema kutokana na hali halisi kwa sababu hivi sasa ukitembelea katika magereza yetu mengi, asilimia kubwa ya wafungwa waweza kubaini kuwa ni wale ambao maskini ya Mungu hata hawajui ni kwanini wamefungwa, na wale ambao walistahili kufungwa, wamejaa mitaani wakibalizi katika viyoyonzi kama wako peponi.

Kwa ujumla ni kuwa nchi hii inakoelekea siko!! Juzi Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini Said Mwema alipokuwa akizungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, aliulizwa swali na mhariri mmoja kuwa afafanue ni wapi ama ni sehemu gani ambayo Jeshi la Polisi na Waandishi wa Habari ambapo wanaweza kukutana kwa heri katika utendaji wao!!! Swali hilo mie lilinipa tafakari ya kina ambayo hata kabla ya kuipatia jibu, ndio nikasikia haya ya Jerry Muro.

Kwa hiyo ni vema tukajiuliza ni kwanini haya yawe hivi! Je yanaukweli ndani yake? Au ndio moja ya njia ya kuwafunga mdomo waandishi?

Au ni sawa na ile Kauli ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliyoitoa Mwanza wakatia wa Maziko ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Antony Mayalla, kuwa yatupasa kujiuliza sisi tulio katika mapambano dhidi ya uovu tu wasafi kiasi gani!!!
Lakini pia bado narudi kwa Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, inadaiwa huyu mshitaki alitoa taarifa kwa polisi kuwa kuna mtu amemuomba rushwa ya sh. milioni 10 na yuko katika mgahawa wa City Garden, nachelea kuaminishwa na Kamanda Kova mtani wangu huyu, eti vijana wake walikosa muda wa kuiarifu TAKUKURU?

Hivi katika hali ya usasa hasa hii ya watu kutanda katika mitandao kama hawana akili nzuri, mtu anaweza kusema kuwa niliona muda wa kukupa taarifa ni mdogo ndio maana nikaamua kufanya hili jambo peke yangu kweli jamani!? hainiingii kabisa akilini. Kamanda Kova aseme ukweli tu wa hii hali, maana taarifa za muro kutiwa mbaloni zilisambaa haraka sana tena zikizungumzia kukamatwa akipokea rushwa ya sh. milioni 10.

Jana nilishangaa kuona hiyo Ten haizungumziwi, kinachozungumziwa ni huo ushaidi usio na kichwa wala miguu ambao sie tuliopembeni tunauona sijui kwa mahakama na Wanasheria wengine wanalionaje hili!?

Any way cha msingi hapa ni kama alivyosema kaka yangu Jessy Kwayu kuwa imefika wakati sasa wa kulisafisha jeshi letu, kama ni kwa kuwapiga chini askari wote jeshi lianze moja au sijui tufanyeje!!

MWEMA NAKUONEA HURUMA HUNA WATU, HUNA WATENDAJI OMBA MUNGU TU AKUZIDISHIE HEKIMA NA BUSARA KAMA ULIVYO SASA, NA ASIKUPATIE UGONJWA WA SUKARI WALA MOYO UTAKAOSABABISHWA NA WATENDAJI WAKO WANOPENDA SIFA!

Mungu atunusuru, nawatakia kazi njema nyote!!!

Mdau Mtaka Haki

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad