HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 5, 2010

Kweli Uswahilini Kuna Vituko!!!!

Huyu dada pichani mchana wa jana huko Magomeni kaenda kumsuta shoga yake kisa,Huyu dada na huyo shoga yake walikuwa ni maswahiba wa kufa na kuzikakiasi kwamba mpaka pamba (nguo) wakawa wanaazimana,sasa huyo shoga yake aliolewa siju za hivi karibuni, na baada ya kuolewa akawa analalamika kuwa bidada huyo hapo pichani anamuonea wivu sana yeye kuolewa kiasi kwamba wakawa wanachuniana hata simu hawapigiani.Maneno yakamfikia mwanadada huyo hapo pichani...,hapo ndipo mbilinge lilipoanza na ndio bidada huyu kukusanya watu na kukodi matarumbeta kwenda kumsuta yule shoga yake.
msela akiselebuka zake kwa raha zake katika kusherehekea usutaji huo
mpiga tarumbeta akiwa mzigoni kusaka zake mahela
goma limenoga
mtaani ilikuwa ni full furaha(sasa sijui walikuwa wanafurahi kuona hilo tukio??).hebu bonyezeni HAPA ukaupate umbea kamili kamili.kweli uswahilini ni noumer.

1 comment:

Post Bottom Ad