
Washtakiwa wa kesi ya kupiga mpaka kusababisha cha Marehemu Swetu Fundikira,wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Geni Vitus Dudu na mashtaka yameendeshwa na wakili wa serikali Monica Mbogo aliyekuwa akisaidiwa na Beatrice Mpangala
Mh. Dudu aliwaeleza washitakiwa hao kwamba kwa mujibu wa kosa linalowakabili hawatakiwi kujibu chochote na kwamba kosa hilo halina dhamana kwa sababu hiyo mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu na kuairisha kesi hiyo Februali 10 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa. Akaamuru washitakiwa wote wamepelekwe rumande.
Ndugu wa marehemu Swetu walikuwepo mahakamani na kusikiliza kesi kwa utulivu, huku wakisema wana imani kwamba haki itatendeka.
Swetu Fundikira alifariki dunia Jumapili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambakoo alilazwa toja Ijumaa usiku baada ya kupigwa sana na wanajeshi watatu, wawili wakituhumiwa kuwa ni hao pichani na mwingine wa tatu haijulikani alipo na msako unaendelea.
Marehemu Swetu alizikwa jana kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar. Kifo chake kimezua zogo kubwa miongoni mwa wananchi ambao wanadai uongozi wa majeshi yote ya ulinzi na usalama uwe wakali kuhakikisha askari wachache wenye mtindo wa nidhamu hawapewi nafasi ya kuchafua majina mazuri waliyo nayo pamoja na ushirikiano mwema kati yao na jamii.
habari na picha ni kwa hisani ya
Sheria ifate mkondo wake
ReplyDelete