HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 6, 2010

Uhalifu Mtandaoni unaoweza Kutokea 2010,Wadau Tuwe Makini Na Haya

Mwaka 2010 ndio uko mwanzoni kabisa pamoja na ni vizuri tuangalia
matisho ya uhalifu unaoweza kufanyika kwa njia ya mtandao kwa mwaka
huu ili wengi wetu waweze kuwa makini zaidi .

Si unajua kwamba mwaka huu kuna Michuano ya kombe la dunia nchini
Afrika ya kusini , wahalifu kadhaa wameanza na wengine wameshafanya
majaribio kadhaa ya kuuza tiketi feki kwa njia ya mtandao au
kumdanganya mtembeleaji wa mtandao aingie kwenye tovuti ambazo ni
bandia kwa kujifanya zina mahusiano na kombe hilo la dunia ni mambo
kama hayo .

Je hili la kusajili namba za simu ? kusajili namba ya simu
inakuwezesha wewe kuwa karibu zaidi na kampuni za matangazo kwahiyo
utegemee kuletewa matangazo mengi sana kwenye simu yako ya mkono na
aina nyingine ya uhalifu kwenye simu hiyo hiyo ya kiganja .

Pia kuna suala la kuangalia sana jinsi tunavyotembelea mitandao ya
jamii kama facebook au hi5 kuna wahalifu wanajificha kwenye mitandao
hiyo kwa majina bandia au kuweka taarifa ambazo sio sahihi kwa ajili
ya kuvutia watu ambao wanaweza kuangukia kwenye mikono ya wahalifu hao
mwishowe kutendewa vitendo viovu .

Ni wakati kwa kampuni mbalimbali zinazoruhusu wafanyakazi wao
kutembelea au kuweka taarifa zao kwenye mitandao hii kuwa na sheria
maalumu zinazohusu mitandao jamii kuweza kutetea maslahi ya kampuni
hizo kwenye mitandao ambayo inahusu jamii kama facebook bila kusahau
kingine kwamba taarifa unazoweka kwenye mitandao hii au picha zako
zinaweza kutumika dhidi yako wakati wowote bila ya wewe kutegemea
kwahiyo ni vitu vya kuangalia sana .

Kwa wale wapenzi wa kutafuta vitu kwa njia ya mtandao kwenye search
engines nao wawe makini sana ni kweli kwamba kuna baadhi ya programu
zinazoweza kutambua tovuti na linki mbaya lakini hili sio kwa asilimia
100 na kwa sasa unaweza kutegeka na majibu unayoyapata kwenye tovuti
hizo ambazo ukitembelea unaweza kudownload program za kuharibu
kompyuta yako na vitu vingine .

Kwa kipindi cha mwaka jana tumeona jinsi uhalifu ulivyofanyika kwenye
mashine nyingi za ATM kwa habari nilizosoma kwenye vyombo kadhaa vya
habari zinasema kwamba Mashine nyingi za ATM zimekuwa na matatizo ya
hapa na pale ila sijasikia matukio mengine zaidi ya kuibiwa pesa kwa
njia hii lakini kuna la kujifunza hapa kwanini Mashine nyingi zinapata
matatizo mara kwa mara ?

Uharibifu wa kitu kama Mashine hizi unaweza kumaanisha uthaifu wa
mashine hizo kwahiyo udhaifu huu unaweza kutumika na wahalifu kwa
ajili ya kufanya mashambulizi makubwa zaidi kwenye mashine hizi na kwa
njia ya mtandao huko mbeleni kwahiyo watu wawe makini sana .

Na mwisho ni kuhusu mwendo wa huduma za mtandao kwa sasa ulivyokuwa wa
kasi kuliko ulivyo huko nyuma , hii inaweza kuvutia wahalifu kwa
njia moja au nyingi na ukizingatia hatuna sheria za masuala ya
mitandao inawezekana kabisa nchi yetu ikageuka shamba la mashambulizi
ya kimtandao kama hali ikiachiwa kuendelea kama ilivyosasa .

Tusisahau mwendo huu wa mitandao umesababisha watu wengi pia waweze
kuchukuwa vitu haswa program nyingi kwa njia ya mtandao ambapo
mitandao mengine inatoa program hizi kwa njia ambazo sio halali hizi
programu zinaweza kuwa na virus ndani au aina nyingine ya programu za
kiuhalifu

Ni vizuri kampuni na mashirika ya ummah kuwa na sera zao zinazohusu
matumizi ya mitandao na vifaa kama komputa na kadhalika ili kuweza
kukabiliana na hali hii kwa sababu kampuni nyingi sana zimekubali
kuuziwa programu hizi pasipo kujua au wafanyakazi wa kampuni hizi
wameuziwa programu hizi pasipo wao wenyewe kujua na matokeo yake ni
kufanya uhalibifu ambao kungekuwa na taratibu nzuri ungeweza
kuzuilika .

Haya ni maoni yangu tu hayahusiani na kampuni yoyote au kikundi
chochote cha watu .

Mdau.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad