HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 18, 2010

Twanga Washindwa Kuwatambia Wazee Wa Ngwasuma Kwenye Kandanda

kikosi cha timu ya Twanga Pepeta kikiwa katika picha ya pamoja
kikosi cha timu ya F.M Academia wazee wa Ngwasuma nacho kikiwa katika picha ya pamojaNyanda wa timu wa FM academia,Nyoshi El Sadaat akimuandalia beki wake mpira tayari kwa kupelekwa mbele kwa wapinzani wao huku straika wa timu ya Twanga Pepeta,Iddy Janguo akiangalia tukio hilo.gemu hili lilimazika kwa kila timu kutomtambia mwenzake yaani bila bila

kikosi kizima cha Twanga kikiimba wimbo wao rasmi kwa mechi hiyo iliyochezwa jana katika viwanja vya Lidaz klabu ambapo hakuna timu iliyoweza kuliona lango la mwenzake kwa dakika zote 90.
Nyanda wa FM Academia,Nyoshi El Sadaat akiwa kwenye jukwaa la washabiki baada ya kuzidiwa na jua wakati akiwa golini.mechi hii ilikuwa ni nzuri sana na kwa matokeo hayo ni kwamba hili gemu litakuja kurudiwa siku nyingene ambayo haijapangwa rasmi kuwa ni lini.mzee wa Mtaa Kwa Mtaa nilikuwepo eneo hilo mwanzo mwisho lakini sikuweza kupata picha za kutosha kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu,hivyo tuvumiliane kwa hata hizi zilizopatikana.

1 comment:

  1. huyo aliyevaa blue si Mwenda? wa Tatu kutoka Kushoto Omari na aliye vaa number 5 si Jigga huyo alisoma Al-haramain? na aliyeshika mpira Iddi Janguo naona wazaramo wamejipendelea hapo.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad