


=== ======= ==== =========== ====== ========= ====== ========
HATIMAYE,kuna habari njema kutoka Zanzibari… Ukiachana na hali mbaya ya kiuchumi ya Dunia iliyoathiri bodi ya Utalii, na ukosefu wa umeme wa muda mrefu, tangu kati kati ya Disemba, hatimaye kuna mtazamo chanya juu ya Tamasha la saba la muziki la Sauti za Busara linalotazamiwa kung’arisha Zanzibar!
“Ni wakati mgumu sana tunajua, lakini juu ya sababu zote! lengo letu ni kusonga mbele, pamoja na Sauti za Busara”, Yussuf Mahmoud anasema, Mkurugenzi wa Busara Promotions. “Tamasha hili ambalo kauli mbiu yake mwaka huu ni MOTO ZAIDI litaleta watu pamoja katika kusherehekea, kuwasaidia vijana wenye uwezo wa kiutamaduni, kuwapa bahati ya kukutana na wasanii wakubwa katika jukwaa moja na kutoa fursa ya kubadilishana mawazo kutoka kwa mmoja kwenda kwa mwingine. Lakini si hivyo tu, Inaweza pia kuwa fursa ya kubadilishana uzoefu, kufahamiana na pia Tamasha la Sauti za Busara linatuwezesha kuboresha utalii mpya wa kiutamaduni nchini Tanzania.”
“Ni kweli”, tumedhamiria kuendelea, “kukosekana kwa umeme kisiwani imetuletea sote wakati mgumu, lakini tumejipanga na majenereta ya kutosha ili kuhakikisha mambo yote yanaendelea kama yalivyopangwa, usalama umeboreshwa na mpangilio mzuri kwa watazamaji. Uukiwepo umeme au ukikosekana, Sauti za Busara iko TAYARI!”
Labda tuwapashe tu kidogo kuwa; Toleo la saba la sauti za busara linaelekea kuleta “habari nzuri” kwa ajili ya Afrika, wasanii kutoka kona mbalimbali za Afrika wanajongea visiwani tayari kwa burudani. Hivi Mahoteli ndani ya mji mkongwe yamekwisha furika, wawezeshaji wa muziki duniani, wanautamaduni pamoja na waandishi wa habari kutoka pande mbali mbali za dunia wako tayari kuja pamoja kushuhudia nini kinaendelea katika mandhari nzuri ya muziki wa Afrika Mashariki.
Tofauti na miaka iliyopita, Sauti za Busara 2010 linakuja na vionjo adhimu, zaidi ya wanamuziki 400 watapanda jukwaa moja. Mbali na vikundi kumi na mbili kutoka Zanzibar na nane kutoka Tanzania Bara, Tamasha hili pia limeshirikisha makundi ishirini kutoka nje ya Nchi kama vile Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Mozambique, Mayotte, Egypt, Guinea, Senegal, Gambia na Zambia.
Kama kawaida, tamasha hili hutokea kipindi cha sikukuu ya wapendanao hivyo kuongeza ladha zaidi. Kutoka viwanja vya watoto Kariakoo saa kumi kamili za jioni siku ya alhamisi tarehe kumi na moja februari kutakuwepo na maandamano makubwa na ya kipekee yatakayo ashiria ufunguzi rasmi wa tamasha hili la aina yake, wakiwemo wana sarakasi, mdundiko, ngoma na bendi, wote wakielekea Ngome Kongwe hadi itakapofika mida ya saa kumi na moja jioni. Kutoka hapo na kuendelea, kutakuwa na shoo za muziki kwa siku nne , pamoja na vikundi 40 (wanamuziki 400) akiwemo Thandiswa(Afrika Kusini), Nyota ndogo na Makadem (Kenya), Ba Cissoko (Guinea), Malick Pathe Sow (Senegal), Massar Egbari (Egypt), Banana Zorro, Fresh Jumbe, Chidi Benz (Tanzania) na wengi wengineo.
Kama kawaida, Tamasha huandaa mikutano na watu wajuzi mbali mbali na wasanii kwa mafunzo ya kiufundi kwa lengo la kuwawezesha watu kupata ujuzi kwa wapenzi wote wa muziki. Februari 16, kutakuwa na sherehe ya kumaliza tamasha zitakazofanyika Jambiani, muziki utakuwepo pamoja na ma DJ wa kimataifa kutumbuiza mpaka asubuhi.
Zantel, ambao ni wadhamini wakuu wa tamasha la saba la sauti za busara wanajivunia kuwaletea tamasha kubwa na la kipekee Afrika ya mashariki, zanzibari kwa mara nyengine tena. Zantel, kampuni ya mtandao wa simu unaotoa huduma ya Internet kwenye simu kwa wateja wake Tanzania na Zanzibari, wanaamini kuwa muziki ni njia nzuri ya kuunganisha maelfu ya waafrika pamoja na watu wengine kutoka mataifa mengine.
Zantel wanafurahi kushirikiana na tamasha la Sauti za Busara na kuutangaza utajili na utofauti wa muziki kutoka Afrika Mashariki. Ni vizuri kutoa jukwaa la kimataifa kuwaonyesha wasanii wenye uwezo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ya masharki
Wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kwa kutangaza tarehe za tamasha na wasanii watakaoshiriki, mkuu wa mauzo Zantel John Mbaga alisema, “Zantel wanajivunia kuwadhamini Sauti za Busara kuleta wasanii mahiri jukwaani ili kuonyesha uwezo na fahari ya Afrika Mashariki duniani kote.
Mpango huu unatupa nafasi sis wote kurudi kwenye asili yetu na kuwapa wateja wetu fursa ya kushuhudia burudani nzuri kwa kipindi kizima cha tamasha. Siku sita za tamasha zitakuwa na zaidi ya vikundi 40 na karibia wasanii 400.”
Zantel wamedhamilia mwaka huu uwe wa mafanikio kwa wasanii wote wa muziki. Wapenzi wa Sauti za Busara na wadhamini, msemo wa mwaka huu wa Pamoja Tunasababisha unafaa kabisa kwenye mada yetu “Pamoja tunasonga mbele
Mpaka kufikia hapa tungependa kutoa shukrani zetu za dhati kwa wadhamini wetu ambao ni: ZANTEL ambao ndiyo wadhamini wakuu wa Tamasha hili,. Sauti za Busara 2010 pia limedhaminiwa na : HIVOS, UNDP, CULTURESFRANCE, Norwegian Embassy, Goethe-Institut, British Council, US Embassy, Alliance Française de Nairobi, Embassy of Germany, Embassy of Denmark, Memories of Zanzibar, ZanAir, Gallery Tours, Fly540.COM, Zanzibar Hotel Group, ZG Design, Ultimate Security na Southern Sun DSM.
Pia tungependa sana kuvishukuru Vyombo vya Habari pamoja na wasanii wote, wafanyakazi wote kwa ujumla kwa kufanya kazi usiku na mchana, kuhakikisha linafanyika. na Wadau mbalimbali walioshiriki kwa namna moja ama nyingine, kulipa tamasha hili ramani yake na heshima inayostahili Zanzibari hapa Tanzania na Duniani kote kwa ujumla.
Tunawakaribisheni sana, shiriki nasi katika kuuwasha MOTO ZAIDI… wa Sauti za Busara 2010.
Kwa habari zaidi,
tafadhali msisite kutemebelea tovuti yetu:
http://www.busaramusic.org/
No comments:
Post a Comment