HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 19, 2010

Machache Toka Kwa Mwana Libeneke King Kif Kuhusiana Na Mauaji Ya Huko Ukerewe

Miaka michache iliyopita niliwahi kusoma kitabu kimoja kinachoitwa Natural Law and Natural Rights (Oxford , 1998) ambacho kimeandikwa na Profesa John Finnis wa Chuo Kiku cha Oxford .

Kwa kifupi ndani ya kitabu hiki kuna masuala yanayohusu uhai, ndoa , mali, elimu, ukweli ,
afya ,burudani na mambo mengine mengi mazuri. Kwa jinsi nilivyosoma kitabu hiki hapa narejea kwa kujenga hoja maridhawa kuhusiana na kanuni za maumbile za mwanadamu na mazingira
yanayomzunguka huku nikitaja mambo yapi ni kweli na yapi si ya kweli kuhusu hulka ya binadamu na mazingira yake.

Hapa kuna mfano kwamba sisi wanadamu wote tunatabia isiyotabirika na hivyo ni lazima tuongozwe na sheria ssiku zote.Tuongozewe na sheria kwa kuwa kuna wakati tunakwepa ama tunavunja tunu za kimaadili kwenye jamii zetu.

Vyombo mbalimbali vya habari vimeripoti kwamba juzi usiku raia 14 waliuwawa na kundi la watu wanaohofiwa kuwa ni majambazi huko Ukerwe huku wengine 17 wakijeruhiwa.
Tukio hili la kusikitisha na kutisha limetokea kisiwani humo kwenye kijiji cha Izinga , watu waliofanya unyama huu ni wenye uchu wa kujipatia mali kwa njia za mkato hatua ambayo ni kinyume cha sheria kama nilivybainisha hapo juu na kukihusisha kitabu cha Profesa John Finnis.

Kanuni za kimaadili nim kanunu ambazo huratibu mienendo huku ikitajwa wazi wazi kwamba yapi yanafaa kufuatwa na kufanywa na yapi si yakufanya kwenye jamii zetu.Kwa mfano ; kuua , kuiba kuzini , kudanganya , kutoa na kupokea rushwa na mambo mengine yasiyofaa kadha wa kadha .sasa basi , kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari , majambazi yakiwa na silaha aina ya Sub Mashine Gun (SMG) yalivamia yalivamia kisiwa hicho kwa lengo la kuwapora wafanya biashara.

Inasikitisha kwamba katika Tanzania hii kuna watu(majambazi) , ambao wanaamini kwamba wanayo haki hewa ya ya kufanya mambo maovu kwa kuvamia na kuua watu!

Tutambue kwamba uhai ni matalaba ya mwanadamu ambayo yanapaswa kuheshimiwa na watu wote kwanye ulimwengu huu , siku zote , sehemu yoyote.Kumuua mtu bila hatia ni uovu , yaani ni kosa na ni uvunjanji wa sheria za nchi na dini pia.

Inatupasa tutambue na tukubali kwamba kila binadamu anao wajibu wa kujiepusha na tendo lolote linalo hujumu matilaba ya binadamu mwenzie kwa makusudi.Uhai ni miongoni mwa matilaba ya binadamu.

Kwa mifano hii kiduchu nadhani nilicho kiandika kimeeleweka .Matendo yanayohujumu matiilaba ya binadamu nii pamoja na kuua , hakuna mtu mwenye haki ya kufanya tendo hili tangu enzi zote na klwenye jamii zote hapa duniani.

Nachukua fursa hii kuwapa pole familia za marehemu huko Izinga,wilayani Ukerewe mkoani Mwanza kwani zimewapoteza ndugu na jamaa wao wapendwa na pia nawapa pole watu wote ambao wamejeruhiwa kwenye tukio hilo.

Nimewakilisha.
Ni mimi KingKif kutoka

www.kingkif.blogspot.com.

Emal;kingkif07@gmail.com.
Simu 0714-077040.

3 comments:

  1. Poleni wafiwa.Kwa sasa ni boraJeshi la Polisi likashirikiana vema na wananchi ili zoezi la kuwasaka na kuwakamata majambazi walifanya tukio hilo la kinyama.Kuna tetesi tayari zimeripotiwa kwamba majambazi hao walifikiaHoteli moja mjni Ukerewe.

    ReplyDelete
  2. Nimesikitishwa sana na tukio hilo na ninaona kuwaWanaukerewe tumeuanza huu mwaka kwa balaa.Naliomba jeshi la polisi lifanye kila jitihada kuwakatata homajambazi.Masatu -Uk.

    ReplyDelete
  3. Napenda kuona uchunguzi wa kina unafganywa kuhusu hao askali wawili ambao wamkamatwa ili haraka iwezekanavyo wafikishwe mahakamani.Ni kosa kubwa kama wasipofikishwa mahakamani halafu eti baadaye tukasikia wamamishiwa sehemu nyingine kikazi!

    ReplyDelete

Post Bottom Ad