Sema wewe Mzee wa Mtaani,
Naomba unisaidie kuniwekea haka ka swali kangu kwa wadau ili waweze kunipatia mchanganuo wa hili swali langu.
Ukiangalia ustaarabu wa zamani basi utakuta kila nchi ama makabila wana kalenda zao. na ufikapo mwaka mpya basi husherehekea. Hata kidini basi kuna dini nyengine zina kalenda zao.
Afrika tumefika mwaka wa ngapi kwa kalenda yetu? ama haipo? Wachina wapo na Kalenda, wakurdi, sijui na watu gani wana kalenda yao. Kidini waislamu wana kalenda yao.
Hata kabila letu sijawahi kusikia kama wanasherehekea mwaka mpya wao! Kalenda ya mtu mweusi inasema huu ni mwaka wa ngapi? Ina maana kalenda ya Gregory imefunika kabisa mwaka wetu kiasi kwamba hatujui hata tunaenda wapi na tunatoka wapi!
Nitarudi tena baadae maana tunazima jenereta kwa sasa.
Mdau Wa Zenzy

No comments:
Post a Comment