HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 23, 2009

RENATHA BENEDICTO UNATAFUTWA NA RAFIKI YAKO

Heshima kwako Ndugu.

Naomba uniwakilishie ombi hili barazani kwako. Namdafuta Dada Mdogo RENATHA BENEDICTO ambaye tumepoteana kwa takriban miaka 7 sasa.

Renatha alikuwa mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kibasila jijini Dar kati ya mwaka 1998 - 2001 na baada ya hapo alienda Songea TTC kujiunga na masomo ya ualimu.

Pia alikuwa kati ya wahanga wa ajali mbaya ya Tawfiq iliyotokea tarehe kama ya leo mwaka 1999 ambapo alikuwa msaada mkubwa saana kuokoa maisha yangu.

Niliwasiliana naye kwa miaka miwili iliyofuata mpaka alipoenda chuoni Songea nami nikaondoka nchini mwaka uliofuata na kwa miaka mingi sasa nimekuwa nikijitahidi saana kumtafuta bila mafanikio.

Naomba kama anaweza kusoma ama kuna anayesoma na kumfahamu anisaidie kuwasiliana naye.

Email yangu ni changamoto@gmail.com
Blessings

www.changamotoyetu.blogspot.com

2 comments:

Post Bottom Ad