HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 21, 2009

Kamjadala

KAKA HABARI YA KAZI
NAOMBA TUJADILI HILI ,HIVI HII SERIKALI YETU INAJUA KUWA KUNA BAADHI YA MAKAMPUNI BINAFSI HAYAWAPI WAFANYAKAZI LIKIZO?
WANALIPA NSSF YA MFANYAKAZI TUU YEYE MWAJIRI HAWEKI?UKIACHISHWA KAZI HUNA UNALOLIPWA?
UKISHITAKI HUNA UNALOPATA KWANI WANAHONGA MNO?
JE TUTAFIKA KWELI?
NI MIMI MDAU MTAA KWA MTAA

6 comments:

  1. Yaani kaka ni kweli hiz kampuni binafsi watu wanafanya kazi miezi 12 bila likizo na hii serikali cjui haijui maana hata Machine inachoka sembuse binadamu mimi naona hili lifuatiliwe maana hawa Mabepari wamezidi Dar es salaam maana mtu hapati likizo yake,Ndo maana hata shule wanafunga kuna likizo ,Kiukweli kila Mfanyakazi anastahili likizo yake kam haendi ujue anaamua yy na anauza likizo yake kwa Mwajiri wake lakini kwa hawa Mapebari sio tunarudi enzi za Utumwa ,Ziko kampuni nyingi hata ukistaki hupati haki yako wanadiriki kusema wanamawakili.Huu si Utumwa jamni Mheshimiwa Chibulunje anajua hili?Waziri Mkuu anajua hili?Tume ya haki za binadamu?Maana hao TWICO hawana lolote ni wala rushwa namba moja kutwa kuja kuvuta hela

    ReplyDelete
  2. kwakwe hii serikali yetu ndio inawaangusha wananchi wake,maana haifatilii kabisa maswala kama haya na iwapo utainua tu mdomo kutaka kuongea lolote basi ujue ndio umeagana na pepo (yaani kibarua ndio kinakuwa kimeota mbawa kabisa) sasa unafikiri utafanyaje na wakati kazi bado unaihitaji???

    ReplyDelete
  3. Yaani kaka Ubarikiwe mno umenigusa ni kweli maana huna hata pakusemea halafu ndo Maisha bora kwa kila Mtanzania haya maana huu ni Unyonyaji live

    ReplyDelete
  4. hivi hawa wahusika wakuu wa inshu hizi yaani namaanisha hao wanyonyaji wanapitia vichapisho kama hivi???

    ReplyDelete
  5. Mimi nadhani Topic kam hiii kaka ungemwomba Mzee walibeneke aweke Comments zote na maada kwani kule hata Muheshimiwa Rais anasoma ,hata Tume ya hakiza binadamu ujumbe utawafikia ,Kak omba Msaa wa Tuta kwa Mzee wa libeneke hata Magazeti waweke hii Link.Ili tutokomeze hwa wanonyaji wasiojali afya za watanzania looh .....Mkereketwa

    ReplyDelete
  6. Hawa mabepari ni kma kunguni maana hawajali Afya za binadamu wenzao jamani hata Machine ina corrupt ikichoka

    ReplyDelete

Post Bottom Ad