HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 30, 2009

Warembo Wa Africa Mashariki Kuanza Kuwasili Wiki Hii

Fatma Abdulahi (20) SOMALIA
Dalysha Nirena Doorga (21) MAURITIUS
Nediat (21) ETHIOPIA
Tabitha (20) KENYA
Asli Osman Mahamud (18).JPG
Rebecca Getachew (23) ETHIOPIA
Fatma Abdulahi (20) SOMALIA
Queen Belle Monique (23) BURUNDI


MISS EAST AFRICA 2009


Warembo wanaoshiriki katika mashindano ya kimataifa ya urembo ya Miss East Africa 2009 wataanza kuwasili Nchini kuanzia wiki hii tayari kwa mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika tarehe 18 mwezi wa 12 katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es salaam.


Aidha, warembo watakaoiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo wanatarajiwa kutangazwa kesho kutwa baada ya kamati maalumu iliyopewa jukumu la kuratibu zoezi hilo kukamilisha kazi yake.

Mashindano ya Miss East Africa mwaka huu yanatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake kutokana na Nchi zinazoshiriki mashindano hayo kuchagua warembo wenye viwango vya hali ya juu ili kuziwakilisha katika mashindano ya mwaka huu.


Miss East Africa 2009 itashirikisha warembo kutoka katika Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, na Mauritius ambazo zote zimeshathibitisha ushiriki wao.

Mashindano hayo makubwa ya urembo kwa ukanda huu wa Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Limited ya jijini Dar es salaam.


Miongoni mwa makampuni yanayodhamini mashindano hayo kwa mwaka huu ni pamoja na Kunduchi Beach Hotel & Resort, EATV, Kings & Queens Worldwide, CMC Automobiles Limited na AKO Catering Services Ltd.


By,

Rena Callist,

CHAIRMAN,

MISS EAST AFRICA PAGEANT

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad