HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 3, 2009

Vodacom Miss Tz 2009/10 Akabidhiwa Gari Lake Rasmi Leo

Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald akiwa amesimama mbele ya gari lake aina ya Suzuki Vitara Grand mara baada ya kukabidhiwa mchana huu kwenye duka la Vodashop mtaa wa Ohio.
Meneja mkuu wa Makampuni ya Shivacom Parthiban C. wa pili kutoka kulia na Meneja wa udhamini na mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza wakimkabidhi funguo za Gari aina ya Suzuki Grand Vitara Vodacom Miss Tanzania Miriam Gerald katika duka la kampuni hiyo lililopo mtaa wa Ohio jijini Dar mapema leo, Gari hilo jipya lenye thamani ya shilingi milioni 53 litamsaidia mrembo huyo katika kazi zake mbalimbali za kijamii .
Miriam Gerald akihojiwa na mwandishi wa habari wa TBC1 Evance Mhando mara baada ya kukabidhiwa gari lake mchana huu.picha na Full Shangwe Blog




Miriam Gerald kutoka Mwanza,alijishindia zawadi hiyo ya gari katika shindano lililofanyika septemba 2 mwaka huu jijini Dar na anatarajiwa kuiwakilisha nchi kwenye shindano la dunia litakalofanyika nchini Afrika Kusini hivi karibuni, anayeshuhudia tukio hilo kushoto ni mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga.

Pamoja na kuzawadiwa mchuma wake,Miriam ataagwa keshokutwa kwenye kituo cha Uwekezaji,TIC kwa ajili ya safari yake ya jijin London Uingrereza na baadaye Afrika Kusini.
Miriam anatarajia kuondoka nchini ijumaa amabapo atashiriki mkutano wa siku tatu wa Kimataifa wa biashara ambao utaanza Novemba 9 hadi 11 nchini humo.

akizungumza hivi karibuni jijini Dar,Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga alisema kuwa wanatarajia mrembo huyo atakwenda kuipeperusha vema bendera ya Tanzania.
Lundenga alisema kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo atakuwa Mkurugenzi wa TIC,Emmanuel Ole Naiko.

Mashindano ya MIss World 2009,yamepangwa kufanyika desemba 12,Sandton Convention Center,mjini Johannesburg.

Mashindano yataanzia London,ambako warembo watawasili Novemba 7,na Novemba 10,watakwenda Dubai,Falme za kiarabu,ambako wataunganisha ndege Novemba 15 kwenda Johannesburg.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad