HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 23, 2009

Mwandishi Wa Habari Alipokutana Na Mkulima

Mkulima amejiwa na Mwaandishi wa magazeti kumuhoji kuhusu maisha ya shambani. Mkulima huyu hawapendi Waandishi wa habari akaona vyema amchoshe katika kujibu maswali, na mambo yakawa hivi:

MWANDISHI: Wewe unawalisha ng'ombe chakula gani?
MKULIMA: Ng'ombe yupi? Mweupe au Mwekundu?

MWANDISHI: Ng'ombe mweupe.
MKULIMA: Ninamlisha nyasi na viguta vya mahindi.

MWANDISHI: Na mwekundu?
MKULIMA: Vilevile nyasi na viguta vya mahindi.

MWANDISHI: ahaa sawa, na sehemu ya kulala ni wapi?
MKULIMA: Ng'ombe yupi? mweupe au mwekundu?

MWANDISHI: Mweupeee!!!!XXCCCZZZZHH!!!!
MKULIMA: Mweupe ninamlaza bomani kulee...

MWANDISHI: na mwekundu?
MKULIMA: Vile vile namlaza na mwenzie.

MWANDISHI: Hii sehemu yote majumba mengi, wakati wa kulisha unafanyaje?
MKULIMA: Yupi mweupe au mwekundu?

MWANDISHI: Woooteeee!!!! [akifuka kwa hasira]
MKULIMA: Mweupe ninamfunga kamba na kumzungusha malishoni na kumrudisha.

MWANDISHI: na mwekundu vilevile?
MKULIMA: Mwekundu? Mwekundu yeye ninamfunga kamba na kuzunguka nae kama mwenziwe tu.

MWANDISHI: Kwanini kila mara nikikuuliza huduma za ng'ombe wako unaniuliza mweupe au mwekundu halafu inatokea kuwa kazi zao wote ni sawa?????
MKULIMA: Kwa sababu ng'ombe mweupe ni wangu.

MWANDISHI: Na mwekundu?
MKULIMA: Na mwekundu ni wangu vilevile.

shuwaini!

1 comment:

  1. yani ni kama namuona mfugaji anavyojibu maswali, nimecheka sana....
    thanks dogo

    ReplyDelete

Post Bottom Ad