
Rais Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda wakipozi na maafisa waandamizi aliowaapisha Ikulu jijini Dar leo ambao wako nyuma yao. Toka shoto ni Sethi Kamuhanda (Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo) Christopher Sayi (Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji), David Kitundu Jairo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Jaji Frederick M. Werema (Mwanasheria Mkuu wa Serikali), Prosper Mbena (Katibu wa Rais), Mbarak M. Abdulwakil (Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi), George Masaju kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye kasimama nyuma kabisa. Nyuma Kulia ni Mh. Peniel Lyimo

Katibu mkuu mpya Wizara ya Habari utamaduni na Michezo Bwana Sethi Kamuhanda akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi katika hafla ambayo Rais aliwaapisha Makatibu wakuu wanne wapya pamoja na Mwanasheria mkuu na Naibu wake

Katibu wa Rais Mpya Bwana Prosper Mbena(kulia) akipongezana na katibu mkuu mpya wa wizara ya Nishati na Madini Bwana David Jairo(kushoto) muda mfupi baada ya hafla ya kuwaapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar leo. Kabla ya uteuzi mpya Bwana Jairo alikuwa Katibu wa Rais
Mzee wa mtaa kwa mtaa naomba ikiwezekana weka hiyo link ukurasa wa mbele nimeinyaka kwenye youtube kaka jinsi pombe isivyokuwa na adabu
ReplyDeletehttp://www.youtube.com/watch?v=JZQsA7G0hvQ&feature=popular
mdau dc