
Mwalimu J.K. Nyerere akiongea kwa msisitizo enzi za uhai wake.

Mwalimu alikuwa ni mpenzi mkubwa sana wa mchezo wa bao,na hapa alikuwa akicheza na mmoja wa wazee waliokuwa ni majirani zake kule nyumbani kwake Msasani huku Mama Maria na Mzee Mwinyi wakiangalia.

Marehemu Baba wa Taifa Mwalim J.K. Nyerere enzi za uhai wake akiwa na viongozi wenzake wa nchi za jirani kipindin hicho,toka kushoto ni Mh. Jomo Kenyata(Kenya ambaye kwa sasa nae ni Marehemu),Mh. Keneth Kaunda (Zambia),Mh. Samora Machel(Msumbiji,nae kwa sasa ni Marehemu),Mh. Robert Mugabe (Zimbabwe) na wa mwisho nimemsahau.
mwili wa Baba wa Taifa ulipowasili na kupokelewa kwa heshima zote,ambapo ulipelekwa uwanja wa Taifa kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho.
umati mkubwa ulifurika katika uwanja wa Taifa siku ya kuaga mwili wa Baba wa Taifa.
BLOGU YETU HII YA MTAA KWA MTAA INAUNGANA NA WADAU WOTE ULIMWENGUNI KUIKUMBUKA SIKU HII AMBAYO BABA WA TAIFA LA TANZANIA MWALIMU JULIUS K. NYERERE ALIYETUTOKA GHAFLA TAREHE 14/10/1999 NA KUTUACHIA MAJONZI YASIYOKWISHA.
MDAU UNAKARIBISHWA KUCHANGIA MAONI YAKO KWA JINSI UNAVYOMKUBUKA BABA WA TAIFA MWALIMU J.K.NYERER KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 10 YA KUKUMBUKA KIFO CHAKE.
PIA UNAWEZA SIKILIZA BAADHI YA HOTUBA ZA BABA WA TAIFA KWA KUBOFYA LINK HII
No comments:
Post a Comment