HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 8, 2009

Dada Astol Mwangomo,Mwanaharakati Anaepigania Elimu Ya Bongo Ifike Mbali

hii ndio Familia iliotoa mchango wa Madawati ya awali
hili ndilo eneo ilipo bustani hiyo
Dada Astol akiwa bega kwa bega na Mafundi kuhakikisha madawati yote yanatengenezwa.
siku ya kukabidhi madawati 33 yaliyotengenezwa kwa msaada mkubwa wa usimamizi wa Dada Astol,hii ilikuwa ni siku ya Graduation ya STD 7.
Wanafunzi wa Shule hiyo wakiimba
hawa ni baadhi ya wanafunzi waliokuwa wamekosa sehemu ya kukaa



ELIMU NI MWANGA WA MAISHA:(BILDUNG IST EIN LICHT DES LEBENS)

Kwanza kabisa napenda kuwasalimu sana wana kijiji wote popote pale mlipo.
Ndugu wana kijiji ni mwaka sasa umekwishapita tangu nilipo Tundika Picha za watoto wa shule ya Msingi Itete,ambao wanakabiliwa na uhaba wa madawati.

Itete Primary School ilianzishwa mwaka 1974,Shule hii inapatikana Mkoani Mbeya -Wilaya ya Rungwe -Tarafa ya Busokelo ktk Kijiji cha Kabembe,Shule hii inakabiliwa na MATATIZO MENGI ,mbayo yamekuwa kama ni kawaida tu kwa Shule zetu hapa Tanzania .

MATAZIZO HAYO NI ,UHABA WA NYUMBA ZA WALIMU :UHABA WA WAALIMU;UCHACHE WA VYUMBA VYA MADARASA HALI AMBAYO HUPELEKEA WATOTO HAO KURUNDIKANA KITIKA MADARASA;NA HILI LA UKOSEFU WA MADAWATI AMBAO HUSABABISHA WATOTO WENGI KUKAA CHINI .Hii imetokana na WAZAZI na WALEZI wengi kushindwa uwezo wa kuchangia PESA za michango hiyo.

Ni wana kijiji wengi waliguswa au kuwaonea huruma sana watoto hao,Wengi wetu walitoa maoni ya tofauti tofauti,Basi hivyo hivyo hata mimi niliguswa haikunipa nafasi ya kukaa kimya,Niliweza kumpata MAMA moja anaye itwa Petra Dammasch,anayefanya maonyesha ya maua wakati wa SUMMER (hapa nchini Ujerumani), ambapo niliongea nae kwa kirefu kuhusiana na jambo hili la kusaidia Watoto hao wa Itete na alikubali na kuniambia kwamba kwa kuwa kila mteja anayekuja hapa huwa analipa €3 basi ktk hizo €3 anazolipa mteja wewe nitakupatia €1 ili kuweza kusadia shule hiyo,Na ndivyo alivyo weza kufanya,Isitoshe baada ya Wateja hawa kumaliza matembezi yao katika bustani hiyo kuna chumba cha kupata Kahawa na Keki ambapo tuliweka( Courage)yaani picha za watoto Ukutani Na KOPO la kutumbukiza Pesa ,Na baadhi yao waliguswa na wakachangia Pia.Lakini Kwa kuonyesha MSISITIZO nilianza kwanza mimi mwenyewe kuchangia na ndipo na wengine waliendelea kuchangia .

Ninachotaka kuwaambia Leo wana kijiji wenzangu ni kwambaa,Katika harakati nilizofanya tumeweza kutengeneza DAWATI 33 tu ambazo ni sawa na watoto 99 sasa wameweza kupata sehemu za kukaa na kusoma vizuri.
Ninaomba tusaidiane katika hili kwa wale watakao guswa na swala zima la elimu katika nchi yetu,ujenzi wa shule bado unaendelea na MADAWATI bado yanahitajika maana bado wanafunzi wengi wanakaa chini.
SHUKRANI ZA DHATI ZIWAENDEE
RHEIDELHOFF GARTEN(FAMILIA DAMMASH)
WALIMU
NA
MAFUNDI

BILA KUSAHAU KIJIJI CHETU CHA
Sisi pamoja na majina ya watoto wote tunawashukuru sana.
(Wir bedanken uns ganz Herzlich im Namen der Kinder).
TUKO PAMOJA
KATIKA KUENDELEZA LIBENEKE LA ELIMU NI MWANGA WA MAISHA
ni
MIMI MDAU MWENZENU

Astol Mwangomo

MUNGU IBARIKI TANZANIA

3 comments:

  1. Nakupongeza sana dada yangu kwa kazi nzuri na moyo mwema ulionao hata ukaweza kuwaza na kwazua namna ya kutafuta njia kama hiyo kunusuru maisha ya watoto kielimu kijijini kwenu.

    Mimi ni mwanakijiji wa Mwakaleli hivyo nimejisikia furaha sana kuona dada yangu unafanya vitu vikubwa kama hivyo.Nakupongeza sana na Namuomba Mungu akuzidishie maarifa na nguvu zaidi ili uendelee kusukuma maendeleo ya elimu kijijini kwetu.

    Kama unaweza kutoa email address yako na namba yako ya simu ningefurahi kuwa na mawasiliano nawe ili tuungane pamoja kusaidiana kupeana mawazo mema kama hayo.
    Ubarikiwe na Bwana ilumbu gwangu.slyasi@yahoo.com
    Mdau USA

    ReplyDelete
  2. Ongera sana dada mungu atakupa zaidi

    ReplyDelete
  3. Safi dada ake wachache wenye moyo kama wako

    ReplyDelete

Post Bottom Ad