SHEREHE YA HARUSI YA KAWAIDA KABISA NIA NA MADHUMUNI NI KUCHANGIA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA MAKALALA-IRINGA-TANZANIA.NAPENDA KUWASIMULIA WADAU WOTE KUHUSU HABARI HII IHUSUYO;
Rafiki mmoja wa hapa Cesena Davide Capponcelli a..k.a (Cappo) ambaye aliamua kufunga ndoa na mtarajiwa wake Mara Tani, mnamo tarehe 15/08/2009 na kuifanya sherehe yake kuwa ya kawaida kabisa bila makuu, lengo lake lilikuwa ni kuchangia kituo cha watoto yatima cha Makalala Children's Home kilichopo Mafinga-Iringa.
Kabla ya sherehe hiyo waliamua yeye na mtarajiwa wake Mara, kuwatangazia wanadungu na marafiki zao wote kuwa; wasiwazawadie chochote bali zawadi na michango yao yote ielekezwe kwa hawa watoto yatima ambao kweli wanahitaji msaada sana, hasa wa afya bora, elimu bora, malezi bora, chakula bora, n.k. kwa kukosa wazazi wao na watu wa kuwatunza. Cappo alifikiri jambo hili la kuwasaidia watoto hawa baada ya kuona haya mwaka jana alipo tembelea kituoni hapo Makalala, na alisema kwanini kufanya sherehe ya kifahari wakati watu wengine wanahangaika na kuhitaji misaada mbalimbali ya kimaisha?
-Kwa bahati mbaya sana sikuweza kuhudhulia sherehe hiyo, kwasababu kipindi cha sherehe hiyo nilikuwa likizo nyumbani Tanzania. Lakini nimemshukuru sana kwa kuonyesha upendo wake mwingi kwa hawa watoto yatima wa nchini kwangu wasio na wazazi, jambo hili limenigusa sana moyoni mwangu, na ndio maana nimependa hata wengine wajue, kwa kuchukua uamzi huu kuwaelezeni wadau wote jambo hili lililo nigusa sana, ili nasi tulio wengi tuinge mfano huu, na kama wapo wengine tayari walishafanya hivi kama huyu jamaa, basi nawapongeza sana na kuwashukuru kutoka moyoni mwangu kwa ukweli.
Harusi ya huyu rafiki alifanikiwa kuchangisha Euro 4000 = Shilingi milioni 7 za (kimatumbi), ili kuwawezesha hawa watoto kwa mambo mbalimbali, ni jambo la kushukuru sana. Basi nasi tufanye sherehe zozote zile si za harusi peke yake, bali sherehe zote zile ziwe za kawaida nzuri bila kupitiliza kiwango kuliko kawaida, kwa kutumia fedha nyingi ili kujionyesha tu kwa watu, na baadae tunajikuta hata sisi wenyewe washerehekea kesho yake tupo kwenye madeni na matatizo mbalimbali, sasa faida yake ni nini?
Shukrani zangu nyingi kwa huyu rafiki na wadau wote hapa na Tanzania kwa ujumla ambao labda tayari walisha onyesha tendo kama hili la upendo wao mwingi kwa kutumia sherehe zao muhimu kwa kuwakumbuka hata na wengine walio na shida za kimaisha ambao tunaishi nao humu humu mitaani na kila siku tonaona walivyo na shida kweli hata kunywa maji tu kunashindikana. Tufanye sherehe nzuri za kawaida, si za kupita uwezo wetu, na zakuonyesha ufahari, bali zinazo kubalika katika jamii na mazingira yetu.
Kwa habari zaidi na picha zaidi unaweza kutembelea hapa:

www.makalala-chibiriti.blogspot.com.
Asanteni sana!
Ni mimi:
Mdau Baraka Chibiriti.
Asanteni sana!
Ni mimi:
Mdau Baraka Chibiriti.
No comments:
Post a Comment