Habari zilizotufikia hivi punde toka pande za Mbagala,zinaeleza kuwa Watoto wawili wamekufa kwa mabomu huko Mbagala Kizuiani karibu na kambi ya jeshi ya kizuiani,wilaya ya Temeka,jijini Dar.
watoto waliofariki ni Reginal Shawala (6) Rajab Said (6),aidha katika mlipuko huo pia kulikukuwepo na majeruhi watatu ambao ni mtoto Sada Seleman (2)Asha Seleman (5) pamoja na Stella Christian Chawala ambaye amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali ya Muhimbili kitengo cha wagonjwa mahututi.
Chanzo cha Mlipuko huo inasemekana ni baadhi ya mabaki ya mabomu yaliyokuwa yamebaki,hivyo familia hiyo ilipokuwa ikifanya usafi katika nyumba yao na kuchoma moto baadhi ya taka taka,ukapelekea mabaki ya mabomu hayo kulipuka.
Aidha Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mh William Lukuvi pamoja na kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar,Afande Suleiman Kova wameeleza kuwa ni kweli tukio hilo limetokea na ni bahati mbaya kwa kilichotokea,hata hivyo taratibu mbalimbali za tukio hilo zinaendelea kufanyika.

1 thing, Waziri wa ulinzi, waziri wa mambo ya ndani, wakuu wa jeshi na vitengo vyao wote wawajibishwe kwa uzembe wa kushindwa kulinda raia na mali zao.
ReplyDeleteUzembe wa kwanza ulifanyika na watu kibao walikufa na wengine wakapoteza makazi yao! Kipi mliwapatia? Pesa za kununua maji! Swali, unaweza kununua uhai wa binadamu kwa pesa? Hatutaki pesa itumike kama kuwafumba macho hawa raia wasio jua haki zao bali tunataka hao wazembe wahusika wafanye kazi ipasavyo ya kuweza kulinda raia na mali zao, kama wakishindwa kufanya kazi wote wakae chonjo.
Tusichezee maisha ya binadamu wenzetu kwa vitu ambavyo vinaweza kuzuilika kabisa, Serikali inabidi ipeleke haraka sana team ya wataalam wa mabomu na kuweza kuyatafuta na kuyaondoa ktk maeneo yote husika. Ni aibu kwa Taifa hili, kila kitu kinachofanyika ndani ya nchi hii ni ujinga ujinga tu!!!! Hakuna Viongozi wenye kujishughulisha, cha maana wao wanawaza ni jinsi gani ya kuweza kuliibia Taifa na raia zake badala ya kuwalinda na kuwatafutia maisha na mazingira mazuri.
Pia tunataka tamko la Serikali ikielezea ni kitu gani kimefanyika tokea mlipuko wa kwanza, juhudu gani zimechukuliwa kuzia matukio haya, Ni wakina nani waliwajibishwa?, Je hamkuweza kufikilia after effects za tukio la kwanza????????????????
Inatia huzuni, Hasira kusikia mpaka leo watu wanapoteza maisha yao kwa kitu kilichotokea mwanzo, Tutajifunza lini? Kama mwanzo mliita bahati mbaya, Hivi sasa nini?
Kikwete please do something NOW Uozo umezidi.