HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 7, 2009

Athari Apatazo Mtoto Pindi Aangaliapo Tv Kwa Muda Mrefu

Watoto wenye kuangalia televisheni kwa zaidi ya masaa mawili kila siku wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa athma. Uchunguzi huo umeonyesha kuwa, kuangalia televisheni kwa muda mrefu kunaleta uwezekano wa kupata athma uongezeke mara mbili kwa watoto.

Jinsi mfumo wa kupumua unavyofanya kazi wakati mtoto anapokaa tu bila kufanya chochote, hupelekea kutokea mabadiliko katika mapafu pamoja na magojwa mengine ya kupumua ikiwemo athma.

Unene wa kupita kiasi pamoja na kutokufanya mazoezi kunakosababishwa na kuangalia muda mrefu televisheni hupelekwa kutokea hali hiyo Wataalamu wamesema kuwa, kuishi maisha ya kutokuwa na harakati yoyote katika umri mdogo hupelekea kuongezeka uwezekano wa hatari ya kupata athma ukubwani.

Hivyo wamewashauri wazazi kuwashajiisha watoto wao kufuata maisha ya kawaida ya kuwa na mishughuliko na kupunguza muda wanaoutumia kuangalia TV.

Wataalamu wa Uingereza wametoa taarifa hiyo baada ya kuwafanyia uchunguzi watoto 3,000 wa nchi hiyo kuanzia wale waliozaliwa mpaka walio na miaka 11.

Athma ni ugonjwa sugu ambao mara nyingi unawapata watoto ambapo hushindwa kupumua, pumzi kuwabana, kukohoa pamoja na kubwana na kifua.kwa mambo haya Afya na mwengine mengi tuu utayapata katika wanja la dada Waridi kwa kubofy link hii http://kona-ya-afya.blogspot.com/

1 comment:

  1. Othman Michuzi Asalaam Alaikum Nenda Google Alafu Click LIFE Dar-es-salaam Picture utaona Picha za Zamani sana DSM wakati wa EID. ukiweza kuzipata wawekee watu waone. Pazi.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad