HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 16, 2009

Uvuvi Mitaroni!!


wanaingia katika ziwa tayari kwa kuvua samaki wa humo ziwani

wamezamisha wavu wao ziwani kusaka vitoweozz kama waonekanavyo
wameibuka na wavu wao ili wacheki idadi ya vitoweozz vilivyopatikana katika ziwa hilo.

kamera ya mtaa kwa mtaa,iliwanasa watoto hawa katika maeneo ya Kijitonyama mbele ya kijiji cha Makumbusho,wakiwa katika mtaro wa maji machafu wakivua samaki,nimejiuliza maswali kibao kichwani mwangu lakini majibu yamepiga chenga,jamani hivi kwenye maji machafu tena yale ya mtaroni huwaga kuna samaki gani?? au ni wale ambao wanapigaga kelele nyakati za usiku??(wale wanaokaa jirani na mitaro kama hii mnainyaka hiyo mili inayotokaga katika mitaro hiyo) maana watoto wa aina hii wapo maeneo mengi sana katika jiji letu hili.

1 comment:

  1. Ingekuwa kwa wenzetu hao wakina dogo lazima wakasomee uvuvi au ubaharia lakii mmmh

    ReplyDelete

Post Bottom Ad