HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 6, 2009

Swali La Kizushiizz!!

Kulikuwa na mlinzi(watch man)aliyekuwa akifanya kazi yake ya ulinzi kwa mzungu mmoja aitwaye Smith.
Bwana smith siku moja akwamwambia mlinzi wake kuwa anatarajia kwenda kwao England siku inayofuatia,mlinzi kusikia hivyo akamwambia bosi wake" bosi bora usisafiri siku uliyo panga maana leo katika ndoto nimeota ndege unayotarajia kupanda imepata ajali na watu wote wamekufa" basi smith akamtii mlinzi wake akaahirisha safari yake, na kweli siku ambayo huyo smith alitarajiwa kusafiri ndege ambayo angepanda ilipata ajali na abiria wote wakafa.Baada ya miezi kadhaa kupita smith akapanga safari tena ya kwenda kwao likizo na alipomjulisha mlinzi wake, mlinzi akamjibu"bosi leo pia nimeota ndege utakayochukuwa kwa siku uliyopanga itapata ajali pia na watu wote watakufa"Smith kusikia hivyo safari hii alichukia akaingia ndani akachukua pesa nyingi tu akampa mlinzi na kumwambi "nenda hakuna kazi tena hapa"

swali! kwanini mlinzi alifukuzwa kazi na wakati utabiri wake ulikuwa unatimia?

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad