Amani, Heshima na Upendo kwako.
Leo ( Aug 10) ni siku nyingine ninayosherehekea mwaka kamili maishani mwangu.
Ninaloweza kukumbuka kwa hakika ni kuwa, katika ukuaji wangu nimekuwa nikijifunza toka kwa wengi. Wenye kunionesha njia kwa kunifunza na wenye kunionesha namna ya kupata njia kwa kunizibia njia. Na kwa namna yoyote ile, nimekuwa nikishukuru kwani naamini ni lazima wote wawepo ili kuweza kujifunza na kukua.
Lakini napenda kukuandikia ujumbe huu kukushukuru kwa mchango wako katika maisha niliyonayo sasa. UMEKUWA KATI YA WALE WALIOANGAZA NJIA KWANGU KWA NAMNA ILIYO RAHISI NA YENYE MSAADA KWANGU. Iwe ni kwa mimi kusoma uandikayo, wewe kusoma niandikayo na kisha kutoa maoni ndani na nje ya "jamvi", ama kwa kuona maisha yako na kupata lililo jipya, naweza kusema kuwa umekuwa msaada kwa namna moja ama nyingine na maisha yangu yako yalivyo kwa kuwa kuna mchango wa yale mema niliyofunzwa nawe.
Napenda kusema kuwa japo sipati nafasi ya kukueleza haya mara kwa mara, lakini naheshimu, nashukuru na pia kubarikiwa saana na mengi nijifunzayo toka kwako.
Tuendelee kuwa na umoja katika kuielimisha na kuikomboa jamii yetu.
PAMOJA DAIMA NA PAMOJA TUTAWEZA
Baraka kwako.
www.changamotoyetu.blogspot.com
No comments:
Post a Comment