HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 6, 2009

Milipuko Yalindima Jiji La Dar Asubuhi Hii

baadhi ya mitungi ya Gas iliyolipuka leo asubuhi huko Kigamboni


Moto uliolipuka kwenye maduka ya kuuzia mitungi ya gesi leo asubuhi huko Kigamboni, jijini Dar es Salaam, ambapo chanzo chake hakikufahamika, umemjeruhi mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Alex na kuharibu mali nyingi katika maduka matatu yaliyo jirani na eneo hilo.Kwa mujibu wa Kamanda Mkuu wa Polisi Mkoa wa Temeke, Liberatus Sabas, moto huo ambao ulianza majira ya saa moja asubuhi katika moja ya maduka hayo ambalo linamilikiwa na Fadhili Rashidi, ulimuunguza vibaya Alex ambaye alikuwemo ndani ya duka hilo.Majeruhi huyo ambaye hali yake inasemekana ni mbaya, amelezwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini.Kamanda huyo alisema moto huo ulihusisha mitungi ya gesi ya kampuni ya Oryx ambayo baadhi yake ilishika moto na kulipuka na hivyo kuusambaza moto katika maduka mengine mawili ya jirani yaliyokuwa yakiuza pia mitungi ya gesi na vifaa vya ofisiniMoto huo ambao ulidumu kwa kiasi cha masaa matatu, ulizimwa na magari ya zima moto ya kampuni ya Ultimate Security kwa pamoja na juhudi za wananchi waliokuwa eneo hilo kabla ya kuenea kwenye maduka mengine yaliyo jirani.Hata hivyo, thamani ya mali iliyoteketea katika moto huo bado haijajulikana.taarifa hii ni kwa msaada wa http://www.globalpublisherstz.com/

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad