HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 31, 2009

Vunja Mbavu:Ajali ya wanasiasa porin

Wanasiasa 40 walipata ajali mbaya sana porini,na baada ya ajali hiyo alitokea mkulima mmoja na alipoona hivyo alichimba shimo kubwa na kuwazika wote kwa pamoja.
Baadaye polisi walikuja eneo la tukio na kumkuta huyo mkulima na kuanza kumhoji kuhusiana na ajali hiyo pamoja na maiti.
na mahojiano yalikuwa hivi:-

Polisi :- Uliona ajali jinsi ilivyotokea?
Mkulima :- Hapana, nilikuta imeshatokea na maiti zimezagaa..
Polisi :- Zipo wapi maiti?
Mkulima :- Nimezizika
Polisi :- Una uhakika wote walikua wamekufa?
Mkulima :- Kuna wengine walikuwa wanalalamika kwamba hawajafa lakini si unajua wanasiasa walivyo waongo, mi nikajua tu wanadanganya nikawazika wote...

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad