
kunradhi wadau lakini naomba niseme wazi kwamba kama si ndesanjo macha hapangekuwa na libeneke na anko nanihii wala asingekuwa nanihii unayemjua leo.
kwa lugha ingine huyu ndiye aliyefanikisha kila kitu katika mambo haya. mtembelee uone vitu vyake kwa kubofya
HAPA na HAPA na HAPA.
ukishamtembelea kote huko utajua ni kwa nini nammaindi sana ndesanjo macha ambaye kwangu mimi ndio kama mama na baba wa libeneke. vile vile ukimsoma ndesanjo macha kwa makini utapata jibu la ufanyeje kuanzisha libeneke la globu pamoja na mambo mengine. huyu mwana wa mfalme wa libeneke hana uchoyo, anapenda kila mmoja wetu aendeleze libeneke...
endapo kama mambo yataenda kama anko nanihii alivyopanga basi kutaandaliwa bash la ubwete kusherehekea hepi besdei ya miaka mitano ya globu ya jamii. kama vipi angalau wadau walitambue hilo, kwamba globu hii inajihisi ina deni kubwa kutoka kwa wadau walioifikisha hapa ilipo.
si jambo dogo ama la masikhara kwani miaka mitano ya libeneke ni umri tosha wa mdau, na kama inavyoeleweka angekuwa mtu basi saa hizi angekuwa darasa la kwanza. na ndivyo globu ya jamii ianavyojisikia kwa sasa. yaani ndio kwanza safari imeanza, na miaka mitano ni cha mtoto.
siku ya siku ikiwadia ya hepi besdei anko nanihii atatoa hutba rasmi, lakini kwa sasa si vibaya kuwashukuru wadau wote kwa kampani yao muda wote huu, kwani safari ina mabonde, miteremko na kashkash kibao ambazo kama una roho ndogo unaweza kuachia bodi.
nawashukuru sana wadau wanaoendeleza libeneke kwa kutuma taswira ama lolote lile ili tushee nao kwenye globu ya jamii. na hapa anko nanihii anaomba kwa unyenyekevu kuweka jambo moja wazi. globu ya jamii haibaugui na wala haichagui. kama mdau una lako jambo ambalo hakichafui hali ya hewa basi litabandikwa tu. likitupwa kapuni ujue umenoa stepu.
halii hiyo ya kutochagua ama kutobagua inalenga sehemu zoteza itikadi iwe dini, siasa, jinsia na hata libeneke la kufurahisha baraza tu. nasema hivi kwa sababu kuna minongóngo kwamba globu hii inapendelea chama fulani tu cha siasa ama imani fulani tu ya dini.
naomba nikanushe tuhuma hizo nzito na kukazia kwamba endapo hao wanaoona hawapewi kipaumbele na globu ya jamii hawaleti taswira na khabari zao kifanyike nini????
hapa kwa ufafanuzi ni kwamba kila jamii iko huru kuleta wakitakacho kwa kutumia
issamichuzi@gmail.com
na kisha endapo kama kitaminywa (na hapa kiwe hakichafui hali ya hewa) ndipo mdau ama muosha kinywa ulalame.
ANGALIZO: globu ya jamii haibagui itikadi ya dini ama siasa, jinsia, aman mada ama libeneke lolote lile lisilochafua hali ya hewa. hivyo endapo wewe ni Mkristo, Mwislamu, Mpagani, CCM, Chadema, CUF, NCCR Mageuzi, TLP na kadhalika lete tutaswira na khabari tuendeleze libeneke. Ila usilalamike wakati wenzio wanaleta wewe unakaa navyo huko uliko.
-Michuzi
No comments:
Post a Comment