1. Pombe za Chimpumu, Dengerua, Kabungusi, Kangara, Komoni, Mbege na Chibuku.
Hupoteza uwezo wa kufikili wa mtumiajiHuongeza ufanisi wa viungo vya mwili vilivyo katikati ya miguu ya mtumiaji chini ya kiuno kwa mbele, hivyo kuongeza uwezekano wa mtumiaji kujiusisha na ngono zisizo salama na kubaka. Zaidi ya 60% ya kesi zote za kubaka zilizotokana na ulevi zimehusishwa na utumiaji wa pombe hizi!Hukakamaza misuli ya midomo na kuongeza ufanisi wa koromeo (voicebox),hivyo si ajabu kuwakuta watumiaji wa pombe hizi wakipayuka ovyo na kwa sauti za juu kuliko kawaida.
2. Pombe za Pingu na Gongo
Hupunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa kufikiri wa mtumiajiHuongeza joto la mwili la mtumiaji kwa kuongeza spidi ya metabolism(metabolic activities), hivyo kuongeza uwezekano wa mtumiaji kuvua nguo hadharani, ili kupunguza joto la mwili!Kwa upande wa pombe ya pingu, hii huongeza spidi ya myeyusho wa chakula(Digestion) na ikitokea mtumiaji hajala kwa muda mrefu huishia kutapika mpaka nyongo. Baada ya kuongeza spidi ya myeyusho wa chakula pombe hii hulegeza vifuniko vya mwili (sphincter muscles) hivyo kuongeza uwezekano wa mtumiaji kuachia kokoo madimba iliyo rojorojo(uharo wa nguvu na wenye harufu kali)Kwa watumiaji wa lile gongo litengenezwalo kwa kinyesi cha binadamu(kigamboni ni eneo maarufu kwa biashara hii), wengi wao huishia Intensive Care Units(ICU), na baada ya hapo hupelekwa Psychiatric Units(wodi za vichaa), kwani zaidi ya 63% ya watumiaji wa pombe hii huishia kuwa vichaa kamili!
3. Pombe ya Mnazi
Kiasi cha ulevi (alcoholic contents) kilichomo katika pombe hii,hushambulia sehemu ya ubongo wa kati (cerebellum), ihusikayo na kutunza utashi, hivyo si ajabu kwa mtumiaji wa pombe hii kuishia kuvurumusha matusi ovyo na kuyumba barabara nzima!Iwapo mtumiaji wa pombe hii hatakuwa mwangalifu na hivyo kunywa mdudu fulani aitwaye kigoto anayekuwa katika pombe hii, basi mtumiaji huyo atakuwa mlevi mbwa wa mnazi maishani mwake!Watu hushauriwa kuviepuka vyoo vilivyotumiwa na walevi wa pombe hii kwani harufu wanayoiacha huko chooni inahusishwa na kuongezeka kwa magonjwa ya saratani ya pua na ubongo (nose and cerebral cancer)
4. Pombe ya Ulanzi
Pombe hii hushambulia viunganishi vya mwili (Body Joints), kwa hiyo asilimia kubwa ya watumiaji wa pombe hii huishia kulala mabarabarani,vyooni na sehemu nyingine zisizo za kawaida kwa kushindwa kutembea!
5. Pombe za Bia, Konyagi. Wiski na Wine mbalimbali
Pombe hizi huongeza hali ya kujiamini kwa watumiaji na pia kuwakumbusha kuwa hapo zamani za kale, waliwahi kupitia shule,hivyo si ajabu kuwakuta watumiaji wa pombe hizi wakizoza kimombo na kujihusisha na mijadala isiyo na kichwa wala miguu punde baada ya kulewa!Pombe hizi hushambulia sehemu zilizo katikati ya miguu chini ya kitovu kwa mbele ya mtumiaji na kuzifanya sehemu hizo kuwa imara na zenye nguvu(strong and active) na hivyo kuongeza uwezekano wa kujihusihsa na ngono zisizotarajiwa na zisizo salama!
SASA KAZI KWAKO KUPAMBANUA!!!
HUU NI UTAFITI WA MDAU CHERRY WA
No comments:
Post a Comment