HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 23, 2008

Sifikilii Kujibizana Na Inspector Haroun - Mwana FA

Ambwene Yesaya a.k.a AY akiwa pamoja Hamisi Mwinjuma a.k.a FA

Msanii wa muziki wa bongo freva,Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ ambaye wiki iliyopita alizushiwa kifo, ameamua kuongea kidogo kuhusiana na ngoma mpya ya Haruna Kahena ‘Inspector Haroun’, ‘Bado upo upo’ ambayo ni kama jibu la wimbo wake, ‘Bado nipo nipo’ kwa kusema kwamba hapendi kujibizana na mchizi huyo, isipokuwa amekerwa na baadhi ya maneno aliyotumia kunako songi lake, ambayo ameyafananisha na matusi.

Akipiga stori na safu hii kwa njia ya simu, Mwana FA alisema kwamba hafikirii kwenda katika vyombo vya habari kwa ajili ya kujibizana na ‘Inspector’, kwasababu alichoimba ni mawazo yake na wala hakuongelea habari za ndoa, wala hakusema watu waachachane kama alivyoimba msanii huyo kutoka TMK.

“Mimi sijazungumzia ndoa, wala kuwataka wanandoa waachane, isipokuwa katika wimbo wangu kuna sehemu nimesema kwamba, watu wanalalamika, wanapoumizwa na ndoa zao, wengine wanaficha, wanakufa na maumivu yao, siwezi kumshangaa sana inawezekana anataka kutokea mgongoni kwangu, lakini kilichonikera ni jinsi alivyonitukana katika wimbo wake,” alisema Mwana FA.

Aidha, Mwana FA alisema kwamba, siku chache zijazo anatarajia kukwea pipa na kwenda kupiga shoo Uingereza na Scotland na mara atakapodondoka Bongo ataachia ngoma nyingine yenye jina la ‘Naongea na Wewe’ ambayo video yake itafanyika nchini Kenya kupitia Kampuni ya Ogopa. “Mpaka mwishoni mwa Oktoba, video na wimbo huo vitakuwa hewani”.
Baadhi ya mashabiki wa muziki wa Bongo Flava waliopiga stori na safu hii, wameikandya tabia ya Inspector kupenda kujibu nyimbo za wasanii wengine kuwa siyo ‘freshi’ na kwamba anaonesha ni jinsi gani alivyoishiwa katika game, kitu ambacho pia kinaweza kumshusha kisanii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad