hii imetokea sasa hivi katika makutano ya barabara ya Sokoine drive na Mission street,ambapo hiyo taxi ilikuwa ikitokea maeneo ya Mamlaka ya mapato (TRA) ikitaka kuingia katika huo mtaa wa Mission street na huyo mwenye daladala alikuwa katika njia yake kama kawaida akitokea posta,ila alikuwa yuko kasi kidongo ndio maana ikafikia hapo.hakuna majeruhi katika ajali hiyo zaidi ya hayo magari kuaribika.hivi itakuwa vipi iwapo na hawa madereva wanaosababisha ajali za kizembe kama hizi,wangekuwa wanayatengeneza wenyewe?maana mara nyingi wamiliki wa magari ndio wanakuwa wanaingia gharama kama hizi.
No comments:
Post a Comment