Kikao cha Tano cha kikundi cha YATIMA WETU kilichotakiwa kifanyike kesho, jumamosi ya tarehe 13/09/2008,pale kijiji cha Makumbusho KIMEAHIRISHWA,hadi hapo kitakapotangazwa tena,kuahirishwa kwa kikao hicho ni kutokana na sababu kuchelewa kwa usajili wa kikundi uliotegemewa kuwa tayari juma hili,lakini hadi siku ya leo usajili bado haujakamilika.
Hivyo tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.Upatapo taarifa hii tafadhali mfikishie na mwanakijiji mwingine.
-Wenu katika ujenzi wa Kijiji
No comments:
Post a Comment