HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, August 29, 2008

Da,Chemi Ndani Edge Of Darkness

Wadau tangu jana nimeigiza katika sinema, Edge of Darkness, hapa Boston. Stelingi wake ni Mel Gibson na Robert DeNiro.
Ninacheza kama askari polisi wa kike (background).
Nitaitwa mara kwa mara kuigiza kwenye background hadi wanapomaliza ku-shuti mwezi Desemba.

Nilipatwa na butwaa nilipopigiwa simu wiki mbili zilizoipita na kuambiwa kuwa nimechaguliwa na mwongoza sinema, kuwa askari kanzu wa kike. Na tena si kwa siku moja tu.Haturuhusiwi kupiga picha kwenye set hii nimepiga mwenyewe Dressing Room.


Ninavaa bastola bandia na madude mengine wanaovaa polisi wa Boston.Mel Gibson mtu poa sana, jana alikuwa anatuchekesha kwenye set, leo alikuja kula lunch kwenye meza tuliyokuwa tunakula. Kaongea vizuri tu na sisi. Tulishangaa kuona mtu "A" list kama yeye anafanya hivyo. Mara nyingi wanaenda kula kwenye trela au hoteli lakini siyo na extras.
Haya nitawapa updates.


Mcheza sinema,
Gbenga Akkinabe (The Wire) mwenye asili ya Nigeria anaigiza kwenye hiyo sinema kama mpelelezi. Nimeongea naye kidogo, alisema kuwa ana marafiki wengi kutoka Tanzania huko New York.

Habari na picha kutoka:
http://swahilitime.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad