HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 25, 2008

Leo Ni Siku Ya kumbukumbu Tanzania

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete leo alishiriki katika kutoa heshima kwa mashujaa walioipigania Tanzania kwa kuweka silaha za asili na maua kwenye mnara wa kumbukumbu za mashujaa uliopo katika Viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es salaam.Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini mbalimbali nchini.Katika hafla hiyo Rais Kikwete aliweka Mkuki na ngao,Sime,Shada la maua,upinde wa mshale pamoja na shoka tukio ambalo pia liliwahusisha viongozi na mabalozi nchini.chini ni baadhi ya viongozi wa juu katika majeshi mbalimbali.picha kwa hisani Haki blog

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad