kutoka kwa mkuu Issa Michuzi wa kijiji cha Michuzi Blog
wadau, hususan wapenzi wa liverpool fc a.ka bwawa la maini. kama nilivyoahidi jana tayari tumeshapata anuani ya barua pepe kurahisisha mawasiliano yetu katika kuanzisha na hatimaye kuendeleza tawi la klabu yetu tuipendayo.
anuani hiyo ni: bwawalamaini@gmail.com
unachotakiwa kufanya kama unataka kuwa memba wa bwawa la maini a.k.a BongoReds kama ambavyo tawi la liverpool la hapa nyumbani litavyojulikana, tuma maelezo yako kwenye anuani hiyo ili uweze kusajiliwa kama mwanachama wa tawi hilo.
idadi maridhawa itapotimia utaitishwa mkutano mkuu ambao utaanza na uchaguzi na kupitisha rasimu ya katiba pamoja na jina rasmi tutaloamua tujiite katika kuendeleza libeneke la bwawani.
hivyo basi
1. tuma jina lako kamili
2. shughuli uifanyayo
3. Jinsia yako na umri wako
4. anuani yako ya kawaida
5. anuani yako ya email
uanachama uko wazi kwa mdau yeyote anayeipenda liverpool
No comments:
Post a Comment