Akizungumza kwa kujiamini bungeni jana, Dk Mwakyembe alisema katika hatua hiyo, ikithibitika kuwa kamati yake ilimwonea mtu katika uchunguzi na mapendekezo yake, yeye na wajumbe wake wako tayari kujiuzulu ubunge na kwamba ikithibitika kuwa ilitenda haki, watuhumiwa wajitoe kwenye nyadhifa zao serikalini.
Pamoja na pendekezo hilo, Mwakyembe alibainisha kuwa kitendo cha baadhi ya wabunge kuzungumzia suala hilo, kinakiuka kanuni za 53 na 54 za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazomzuia mbunge kukumbushia mambo ya Bunge yaliyojadiliwa na kutolewa maamuzi.
Pendekezo: Kama wapo wasioridhika na maamuzi ya Richmond tutengue kanuni hizo ili tuendeshe mjadala mwingine kusudi watu waseme na sisi (kamati) tuseme yote hata ambayo hatukuyasema kwa heshima ya serikali,? alisema Mwakyembe.
Dk Mwakyembe alikuwa anatoa mchango wake katika mjadala wa kuchangia Bajeti ya Waziri Mkuu, akiwakumbusha wabunge kuwa kamati yake iliundwa kwa uamuzi wa Bunge, hivyo kitendo cha baadhi ya wabunge kuwasafisha watuhumiwa wa Richmond
ni kulidhalilisha Bunge.
?Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie kero moja, ambayo ni michango ya baadhi ya wabunge kukosoa maamuzi ya kamati kuhusu Richmond. Badala ya kuzungumzia mambo ya msingi watu wako 'busy kusafishana'. Unamsafisha nani?? alihoji Mwakyembe.
Alisema baadhi ya wabunge wanadhani kuwa uamuzi wa Richmond ni wake (Mwakyembe) na hivyo wako huru kuukosoa na kusahau ukweli kwamba Bunge linaulinda kwa kanuni.
Alisema baadhi ya wabunge wanadhani kuwa uamuzi wa Richmond ni wake (Mwakyembe) na hivyo wako huru kuukosoa na kusahau ukweli kwamba Bunge linaulinda kwa kanuni.
?Tukikutwa tulimwonea mtu, tuko tayari kujiuzulu ubunge, lakini ikithibitika tulikuwa kweli, wahusika wajitoe kwenye nyadhifa zao serikalini,? alisema.
Wakati Mwakyembe akitoa msimamo huo, wabunge walionekana kuwa makini zaidi kusikiliza hoja zake tofauti na mwanzoni alipokuwa akijitambulisha rasmi kwamba amerudi bungeni na afya yake inaendelea vizuri.
?Nawashukuru watu walioniombea pamoja na homa yangu kutiwa chumvi sana ambapo wengine walisema nimefariki, lakini namshukuru Mungu afya yangu inaendelea vizuri,? alisema Dk Mwakyembe kabla ya kuanza kutoa mchango wake.
Katika mchango wake Dk Mwakyembe pia aliishauri Serikali kuhamisha Kitengo cha maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ili kuongeza ufanisi.
Aliema kitengo hicho kihamishwe na kiajiri wastaafu wa JWTZ ambao watafanya kazi kwa ufanisi zaidi kuliko ukiritimba unaofanywa na Kitengo cha Maafa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu.
?Mheshimwa Mwenyekiti kitengo cha Maafa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu kimejaa ukirimba wa kiraia. Kazi waliofanya wanajeshi kujenga daraja mkoani Mbeya kwa siku nne, ingefanywa kwa hata miezi minne na kitengo cha maafa,? alisema.
Sakata la Richmond lilibadili hali ya siasa ya nchi kufuatia maamuzi ya mazito ya Mkutano wa Mumi wa Bunge, na kusababisha aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, alijiuzulu baadha ya kutajwa kwenye ripoti ya kamati hiyo.
Katika uchunguzi uliofanywa na Kamati Teule ya Bunge chini ya Dk Mwakyembe, ulibaini nafasi ya waziri mkuu ilishindwa kuwajibika kuzuia ufisadi huo.
Baada ya kujiuzulu Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamgi na aliyekuwa Waziri wa Afrika Mashariki Dk Ibrahim Msabaha awali alikuwa Waziri wa Nishati na Padini, pia walijiuzulu.
Maamuzi hayo yalisababisha yalimfanya Rais Jakaya Kikwete avunje Baraza la
Baada ya Rais kuvunja baraza, Cunge lilitoa mapendekezo 23 kwa serikali ambayo yalipaswa kufanyiwa kazi ambayo baadhi ni kutaka wahusika wote wa mkataba wa Richmond, wachukuliwe hatua na kwamba malipo dhidi ya kampuni hiyo yasitishwe.
Hata hivyo, tangu maamuzi ya bunge katika mkutano huo wa 10 kumekuwa na juhudi mbalimbali za kuwasafisha watuhumiwa wa Richmond akiwemo Lowassa.habari hii ni kwa hisani ya www.mwananchi.co.tz
Kazi ipo kweli kweli hapa. Siku moja bakora zikitembezwa naona ndio serikali yetu itajifunza.
ReplyDeleteNampongeza sana Dr. Mwakyembe na kamati yake, sasa tena waseme hata hayo waliyoyaacha kwa kuwaona hutuma kina RICHMOND.
Mama Malaika