
Mwenyekiti wa baraza la michezo nchini BMT Idd Kipingu, katikati, akifafanua jambo kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha watanzania kwenda kuishangilia timu hiyo kwenye pambano la kimataifa na Mauritius litakalofanyika jumamosi wiki hii kwenye uwanja mpya wa taifa jijini Dar es Salaam, hafla hiyo ilifanyika kwenye ofisi za shirikisho la soka Tanzania (TFF) jana, kushoto ni Afisa habari wa Kampuni ya Serengeti Bia(SBL) Tedy Mapunda na kocha mkuu wa Stars Macio maximo.

Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Juma Kapuya akisalimiana na warembo walioandaliwa na kampuni ya Serengeti Bia Kuhamasisha Watanzania kwenda kuishangilia timu hiyo kwenye pambano la kimataifa na Mauritius litakalofanyika jumamosi wiki hii kwenye uwanja mpya wa taifa jijini Dar es Salaam, hafla hiyo ilifanyika katika Soko la Karume karibu na ofisi za shirikisho la soka Tanzania (TFF) jana.
Well, all I can say is. Im hungry.
ReplyDelete