mimi ya kwangu ni kama hiyo ya mama Theresa,wewe je?
Kuna mtu mmoja alifariki dunia na akaenda kwa Mungu,alipofika akakuta saa za ukutani nyingi sana zimetundikwa.
Akauliza "Hivi hizi saa ni za nini huku?" Akajibiwa na Askofu mkuu aliyemkuta huko, "Kila saa ina dhambi za kila Binadamu,ikizunguka mara moja ina maana ametenda dhambi mara moja".
Yule jamaa akauliza "mbona hii hapa imesimamani mbovu?
Akaambiwa hiyo ni ya mama Theresa, na inamaanisha kuwa hakutenda dhambi kabisa ndio maana imesimama
Jamaa ikabidi aulize tena, Hivi saa ya George Bush iko wapi kati ya hizi?
akajibiwa ya Bush iko ofisini kwa Bwana Yesu mwenyewe maana anaitumia kama feni kwa jinsi inavyozunguka mara nyingi na kwa kasi
No comments:
Post a Comment