HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 8, 2026

MCHENGERWA AWATAKA WANANCHI KUJIUNGA NA BIMA YA AFYA KUPUNGUZA MZIGO WA GHARAMA ZA MATIBABU

Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amewasisitiza wananchi kote nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kukata bima ya afya ili kujipunguzia mzigo wa gharama kubwa za matibabu ambazo zimekuwa zikiwaelemea wananchi wengi pale wanapougua ghafla bila kuwa na uwezo wa kifedha.

Agizo hilo amelitoa leo, Novemba 8, 2026, alipofanya ziara ya kikazi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili- Mloganzila  iliyolenga kukagua hali ya utoaji huduma na kuzungumza na   wagonjwa  kujua changamoto wanazopitia wakati wa kupatiwa matibabu.

Mheshimiwa Mchengerwa amefafanua kuwa nia ya dhati ya Serikali ya awamu hii ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora, za uhakika, na kwa wakati bila kujali hali yake ya kiuchumi na kusema kuwa mkakati wa sasa ni kuimarisha mifumo ya bima ili kuelekea kwenye mpango wa bima ya afya kwa wote, ambao utamaliza kabisa changamoto ya wananchi kukosa matibabu kwa sababu ya ukata.

Kufuatia ziara hiyo, Waziri ametoa wito kwa watendaji wa sekta ya afya na mashirika ya bima kuongeza kasi ya uelimishaji na kusogeza huduma za usajili karibu zaidi na jamii. Amehimiza kuwa na bima ya afya sio anasa, bali ni uwekezaji muhimu katika kulinda afya na uchumi wa familia zote nchini. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad